Pata taarifa kuu
UINGEREZA-EU-USHIRIKIANO-UCHUMI

Brexit: May akabiliwa na shinikizo la kutosaini makubaliano ya kudumu ya forodha

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May anakabiliwa na shinikizo kutoka chama chake cha Conservative, ambacho kinamtaka aachane na wazo la maelewano na upinzani kuhusu Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya.

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May, baada ya kushiriki katika mkutano kuhusu kusogezwa mbele mchakato wa Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya Aprili 11, 2019.
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May, baada ya kushiriki katika mkutano kuhusu kusogezwa mbele mchakato wa Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya Aprili 11, 2019. REUTERS/Eva Plevier
Matangazo ya kibiashara

Karibu miaka mitatu baada ya uamuzi wa Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya kupitia kura ya maoni, wanasiasa nchini Uingereza hawajakubaliana kuhusu tarehe ya Uingereza kujitoa rasmi katika umoja huo.

Mchakato huu wa Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya ulitarajiwa kufanyika Machi 29 mwaka huu, lakini Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May, alishindwa kupata uungwaji mkono kutoka bunge kuhusu makubaliano yake na Umoja wa Ulaya. Kwa hiyo aliomba chama cha upinzani cha Labour kinachoongozwa na Jeremy Corbyn, kumuunga mkono.

Mawaziri wa zamani kumi na tatu wa serikali ya Uingereza, pamoja na Graham Brady, mwenyekiti wa Kamati ya 1922, ambayo inajumuisha wabunge kutoka chama cha Conservative wasio mawaziri wamemwandikia barua Theresa May wakimtaka kutokubali ombi la chama cha Labour, ambacho kinataka Uingereza kuendelea kusalia katika umoja wa forodha na Umoja wa Ulaya baada ya nch hiyo kujitoa katika Umoja wa Ulaya.

"(La sivyo) utapoteza imani ya chama cha Conservative (...). Tunakuomba kufikiria upya, " barua iliyochapishwa kwenye gazeti la The Times imebaini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.