Pata taarifa kuu
Uhispania-UCHAGUZI-SIASA

Chama cha Kisoshalisti chashinda uchaguzi Uhispania

Waziri mkuu wa Uhispania, Pedro Sanchez anayeongoza chama cha Kisocialisti, ameshinda uchaguzi wa mapema uliofanyika jana Jumapili kwa kupata idadi kubwa ya viti, idadi ambayo hata hivyo atalazimika pia kushirikiana na vyama vingine.

Waziri Mkuu wa Uhispania, Pedro Sanchez, afurahia ushindi wake, Madrid, Aprili 28, 2019.2019.
Waziri Mkuu wa Uhispania, Pedro Sanchez, afurahia ushindi wake, Madrid, Aprili 28, 2019.2019. REUTERS/Sergio Perez
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huo ambao uliitishwa mapema zaidi kabla ya muda na waziri mkuu Sanchez, ulikuwa ni kipimo kwa chama chake, huku ukishuhudia vyama vya mrengo wa kulia vikiongeza viti.

Licha ya kupata idadi ya viti ambavyo vinamuwezesha kuunda Serikali peke yake, waziri mkuu Sanchez atalazimika kushirikiana na vyama vingine vilivyopata idadi kubwa ya viti ili kuwa na umiliki kamili kwenye bunge.

Vyama vya mrengo wa kushoto ambavyo vilikuwa kimya tangu kuangushwa kwa utawala wa kifalme wa Francisco Franco mwaka 1975, vimepata asilimia 10 ya viti bunge kwa mara ya kwanza.

Chama cha Popular ambacho kimekuwa kikiendesha harakati za misimamo mikali na kujitenga kwa eneo la Catalonia, kimepata pigo vaada ya kupata viti 66 kutoka viti 137 mwaka 2016.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.