Pata taarifa kuu
UINGEREZA-EU-USHIRIKIANO-SIASA

Brexit kusogezwa mbele kwa miezi 12

Rais wa Baraza la Ulaya Donald Tusk anatarajia kupendekeza mchakato wa Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya kusogezwa mbele kwa miezi 12 kuanzia tarehe ya Brexit, shirika la Habari la Reuters limenukuu chanzo cha Ulaya.

Donald Tusk (kushoto), Rais wa Baraza la Ulaya pamoja na Rais wa Tume ya Ulaya Jean-Claude Junkcer, tarehe 17 Februari 2016 Brussels.
Donald Tusk (kushoto), Rais wa Baraza la Ulaya pamoja na Rais wa Tume ya Ulaya Jean-Claude Junkcer, tarehe 17 Februari 2016 Brussels. REUTERS/Yves Herman
Matangazo ya kibiashara

Ufumbuzi huu, ambao unahitaji idhini ya viongozi 27 wa Umoja wa Ulaya watakaokutana wiki ijayo, utaruhusu Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya mara tu ya London kutia sahihi mkataba uliofikiwa kati ya Waziri Mkuu Theresa May na viongozi wa Brussels.

"Njia pekee ya busara ni ile ya kusogeza mbele mchakato huo kwa muda mrefu lakini rahisi.

"Tunaweza kupendekeza kwa Uingereza mchakato wa Brexit kusogezwa mbele kwa mwaka mmoja, ambao utakuwa umekamilika baada ya Baraza la Wawakilishi kukubali na kutia saini kwenye mkataba wa Uingereza kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya," chanzo hicho ambacho hakikutaja jina kimeongeza.

"Na ikiwa haikuwezekana, Uingereza inaweza kuwa na muda wa kutosha wa kufikiria upya mkakati wake wa kujitoa katika Umoja wa Ulaya."

Wadadisi wanasema kujitoa kwa Uingereza kumechangiwa kwa sehemu kubwa na kile ninachoendelea Ulaya ambapo baadhi ya wanasiasa wamekuwa na tabia ya kupenda siasa za kihafidhina, za uzalendo , kuzuia mwingiliano na wengi hasa wanaotoka nje ya Ulaya.

Iwapo mkataba huo hautapitishwa, kuna hatari ya Uingereza kujiondoa kwenye Umoja huo bila ya mkataba wowote Aprili 12.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.