rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Uingereza EU Theresa May

Imechapishwa • Imehaririwa

Theresa May kuomba kuongezwa muda wa nchi yake kujiondoa EU

media
Mjadala kuhusu Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya, Januari 16 katika Bunge la Ulaya, Strasbourg. REUTERS/Vincent Kessler

Waziri Mkuu wa Uingereza Bi Theresa May anatarajiwa kuwaandikia barua wakuu wa Umoja wa Ulaya, kuwoamba, waiongoezee muda nchi yake, kuelekea kujiondoa kwenye Umoja huo.


Hatua hii inakuja, baada ya wabunge kukataa mapendekezo ya serikali yake ya namna ya kujiondoa kwenye umoja huo.

Kumeripotiwa mvutano katika baraza la mawaziri, huku kukiwa na wasiwasi kuwa huenda Uingereza ikachelewa kujiondoa hata kwa muda wa miaka miwili.

Michel Barnier amekuwa akiwakilishaa Umoja wa Ulaya kwenye mazungumzo ya Uingereza kujiondoa.