rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Uingereza EU Theresa May

Imechapishwa • Imehaririwa

Brexit: May aendelea kubanwa koo

media
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May, MAchi 12, 2019 mbele ya wabunge. UK Parliament/Mark Duffy/Handout via REUTERS

Spika wa bunge nchini Uingereza John Bercow amesema hatakubali mapendekezo mengine kupigiwa kura kuhusu nchi hiyo kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya, iwapo Waziri Mkuu Theresa May hatawasilisha mswada mpya kwa wabunge.


Uamuzi huu unaendelea kumpa wakati mgumu Waziri Mkuu May, ambaye wiki iliyopita, mapendekezo yake yalikataliwa na wabunge wakati huu muda wa kujiondoa kwenye Umoja huo ukikarabia kufika.

Spika Bercow amesema mswada uliopingwa hauwezi kurudishwa bungeni bila ya kufanyiwa marekebisho.

Wabunge nchini Uingereza wanataka Umoja wa Ulaya kutoa muda zaidi, kuwezesha majadiliano ya mkataba utakaokubaliwa na kila mmoja.