Pata taarifa kuu
UFARANSA-KANISA-HAKI

Kardinali Barbarin ahukumiwa kwa kushindwa kukemea vitendo vichafu

Kiongozi wa kanisa Katoliki nchini Ufaransa, Kardinali Philippe Barbarin amehukumiwa leo Alhamisi Machi 7 na Mahakama ya Jinai ya Lyon kifungo cha miezi sita jela.

Kardinali Barbarin ametangaza kujiuzulu kwenye nafasi yake katika mkutano na waandishi wa habari huko Lyon tarehe 7 Machi 2019.
Kardinali Barbarin ametangaza kujiuzulu kwenye nafasi yake katika mkutano na waandishi wa habari huko Lyon tarehe 7 Machi 2019. JEAN-PHILIPPE KSIAZEK / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mahakama imempata na hatia ya kushindwa kukemea na kukaa kimya kwa vitendo udhalilisha dhidi ya watoto kwa kasisi wa dayosisi yake. Saa chache baada ya uamuzi huo wa mahakama, Kardinali Barbarin ametangaza kwamba anatarajia kukabidhi barua ya kujiuzulu kwa Papa Francis.

Mahakama ya Ufaransa imempata na hatia kiongozi wa ngazi ya juu katika kanisa nchini humo na kumhukumu kifungo cha miezi dita jela.

Wakati wa hukumu hiyo, huyoKardinali Barbarin hakuwepo.

Jajai mkuu wa Mahakama ya Jinai ya Lyon, Brigitte Verney, "amempata na hatia ya kushindwa kukemea kitendo kichafudhidi ya mtoto mmoja kati ya mwaka 2014 na 2015.

Wanasheria wa Kardinali Barbarin wametangaza kuwa wakata rufaa. "Hoja ya mahakama haiiniingia akilini. Kwa hiyo tutapinga uamuzi huu kwa njia zote muhimu za kisheria, "amesema Jean-Felix Luciani, akibainisha kuwa" ilikuwa vigumu kwa mahakama kukataa shinikizo hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.