Vizibao vya Njano: UN yaomba uchunguzi kuhusu "matumizi ya nguvu za kupita kiasi
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu imeitaka Ufaransa "kufanya uchunguzi wa kina" kuhusu machafuko ya polisi wakati wa maandamano ya "vizibao vya njano" tangu mwanzoni mwa mwezi Novemba mwaka jana.
Imechapishwa:
Katika hotuba ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu mjini Geneva, Michelle Bachelet amesema kuwa "vizibao vya njano" wanaandamana dhidi ya "kile wanachoona kama kutengwa kwa haki za kiuchumi na kushiriki katika masuala ya umma ".
"Tunaiohimiza Serikali kuendelea na mazungumzo na tunaomba kufanya haraka uchunguzi wa kina kuhusu kesi zote zinazohusiana na matumizi ya nguvu za kupota kiasi," ameongeza Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu.
Michelle Bachelet amekumbusha kuwa "nchi karibu zote zinakumbwa na suala ka kutofautiana" na hata "katika nchizilizostawi kiuchumi, watu wanajihisi kuwa wametengwa kwa faida za maendeleo na kunyimwa haki za kiuchumi na kijamii".
Starting now at #HRC40: UN Human Rights Chief @mbachelet presents global update on the activities of the Office and recent #HumanRights developments.
UN Human Rights (@UNHumanRights) March 6, 2019
Watch LIVE 📺 https://t.co/JInciPe1QV