Pata taarifa kuu
UFARANSA-HAKI

Ufaransa: Magereza yafungwa baada ya mfungwa kushambulia askari magereza

Siku moja baada ya mfungwa mwenye msimamo mkali kushambulia askari magereza wawili, jela ya Alençon / Condé-sur-Sarthe imefungwa tangu Jumatano asubuhi na maafisa wa jela hilo. Hali hiyo pia imezikumba jela kadhaa nchini Ufaransa.

Askari magereza wakiongea na wenzao walioweka vizuizi kwenye lango la jela la Condé-sur-Sarthe, Machi 6.
Askari magereza wakiongea na wenzao walioweka vizuizi kwenye lango la jela la Condé-sur-Sarthe, Machi 6. JEAN-FRANCOIS MONIER / AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika Magereza 18, kati ya 188 nchini Ufaransa, askari magereza wameamua kusitisha kutoa huduma, mamlaka ya magereza imebaini. Mbali na jela ya Condé-sur-Sarthe, mgomo huo umeyakumba magereza ya Fleury-Mérogis, Melun, Tarascon, Gradignan, na Borgo. Pia hatua kadha zimechukuliwa katika magereza mengine.

Maafisa wa magereza wanapinga kile wanachosema kushambuiwa kila mara na wafungwa.

Chanzo kutoka mamlaka ya magereza, kimebaini kwamba tangu mwanzoni mwa mwka huu, vyama vya maafisa wa magereza vimeorodhesha kesi 101 za kushambuliwa na wafungwa

Katika jela la Fleury-Mérogis, karibu na Paris, jela kubwa zaidi barani Ulaya,vizuizi vimeondolewa asubuhi na vikosi vya polisi, baada ya barabara inayoingia katika jela hiyo kufungwa na wananchama wa chama cha askari magereza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.