Pata taarifa kuu
UFARANSA-SYRIA-USALAMA

Novemba 13: Mwanajihadi Fabien Clain, sauti ya IS, auawa Syria

Fabien Clain, mwanajiahdi, raia wa Ufaransa, ambaye sauti yake ilitambuliwa katika ujumbe wa madai ya kundi la Islamic State kuhusu mashambulizi ya Novemba 13, 2015 jijini Paris na Saint-Denis, ameuawa nchini Syria.

Polisi na maafisa wa kikosi cha Zima Moto wakipia doria katika eneo jirani na Bataclan, Novemba 13, 2015.
Polisi na maafisa wa kikosi cha Zima Moto wakipia doria katika eneo jirani na Bataclan, Novemba 13, 2015. REUTERS/Christian Hartmann
Matangazo ya kibiashara

Fabien Clain aliuawa katika mashambulizi ya anga ya muungano wa kimataifa unaoongozwa na Marekani, kwa mujibu wa Franceinfo. Ndugu yake Jean-Michel alijeruhiwa vibaya.

"Kwa ajili ya Allah, tunajitoa muhanga. Kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, tutwaangamiza "Jean-Michel na Fabien Clain walisema katika moja ya video za propaganda za kundi la Islamic State iliyorushwa wiki chache baada ya mashambulizi ya Paris. Siku moja baada ya mashambulizi hayo ya Novemba 13, Fabien Clain alisifu mashambulizi hayo akisema "mashambulizi yaliyobarikiwa" ambayo yaliendeshwa na "askari wa IS" katika "mji mkuu wa watu waliopotea kiimani."

Fabien na Jean-Michel Clain, wanaofahamika kwa majina ya Omar na Abdelwahid, 40 na 38, walikuwa na uhusiano wa karibu na Mohamed Merah, mhusika mkuu wa mauaji ya Toulouse na Montauban.

Merah, mkatoliki, na mkaazi wa eneo la Reunion, aliingia Uislamu katika miaka ya 1990.Tangu wakati huo, katika eneo la Mirail huko Toulouse, walikuwa ni watu wenye msimamo mkali wa kidini. Mnamo mwaka 2006, walikamatwa na mahakama kwa kujaribu kwenda kujiunga na wanajihadi wengine nchini Iraq. Miaka tisa baadaye, waliweza kuingia nchini Syria pamoja na familia zao.

Fabien Clain aliteuiliwa kuwa msemaji wa kundi la IS kwa lugha ya Kifaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.