Pata taarifa kuu
UFARANSA-MAANDAMANO-SIASA-KODI

Maandamano mapya yashuhudiwa katika miji mbalimbali nchini Ufaransa

Waandamaji karibu 50,000 wakiwa wamavalia mavazi ya njano, walianza tena maandamano mapya nchini Ufaransa siku ya Jumamosi.

Maandamano jijini Paris nchini Ufaransa, Jumamosi 5 2019
Maandamano jijini Paris nchini Ufaransa, Jumamosi 5 2019 REUTERS/Gonzalo Fuentes
Matangazo ya kibiashara

Kulishuhudiwa makabiliano makali kati ya waandamaji na polisi jijini Paris, huku wakiteketeza pikipiki na kuziba barabara kuu ya Boulevard Saint Germain.

Polisi kwa saa kadhaa, walitumia mabomu ya kutoa machozi kuvunja maandamano hayo, ambayo yalisababisha kukwama kwa shughuli katika maeneo kadhaa ya jiji hilo kubwa nchini Ufaransa.

Maandamano haya yamekuwa yakifanyika tangu mwezi Novemba mwaka 2018, ambapo raia wa nchi hiyo wanalalamikia kupanda kwa gharama ya maisha na yalianza kupinga kodi mpya ya nyongeza kwa bidhaa ya mafuta.

Rais Emmanuel Macron kwa nyakati tofauti amejaribu kuwashawishi waandamaji kuachana na maandamano hayo huku akiahidi kushughulikia madai yao lakini kwa maandamano ya Jumamosi, ni ujumbe kuwa yataendelea kushuhudiwa zaidi mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.