Pata taarifa kuu
URUSI-UFARANSA-MAANDAMANO-USHIRIKIANO

Moscow yakanusha kuhusika katika maandamano Ufaransa

Urusi imekanusha kuhusika katika maandamano yaliyotokea Desemba 8 nchini Ufaransa. Kwa mujibu wa msemaji wa Kremlin, madai yoyote yanayosema kuwa Urusi ilichangia kuchochea maandamano dhidi ya serikali ya Ufaransa ni uzushi.

Msemaji wa Kremlin Dmitri Peskov.
Msemaji wa Kremlin Dmitri Peskov. Alexander NEMENOV / AFP
Matangazo ya kibiashara

Urusi inalaumiwa katika uchunguzi wa Sekretarieti kuu ya Ulinzi na Usalama wa Taifa. Mamlaka nchini Ufaransa wanakiri kuwa walifanya uchunguzi kuhusu uwezekano wa Urusi kuingilia katika kuchochea maandamano yanayoendelea nchini Ufaransa kupitia mitandao ya kijamii.

Madai ambayo Dmitry Peskov, msemaji wa Kremlin, amefutlia mbali.

Urusi inaona kwamba kinachotokea nchini Ufaransa ni jambo pekee la ndani.

"Hatuna faida yoyote ya kuingilia mambo ya ndani ya nchi yoyote, ikiwa ni pamoja na Ufaransa" maesema msemaji wa Kremlin.

"Tunashikilia umuhimu mkubwa kwa maendeleo ya uhusiano wetu na Ufaransa. Katika suala hili, nchi zetu mbili zinafanya kazi kwa bidii. Tunaheshimu uhuru wa Ufaransa. Madai yoyote ya uwezekano wa Urusi kuingilia katika masuala ya ndani ya ufaransa ni uzushi, " ameongeza Dmitri Peskov.

Tangu maandamano hayo yalipoanza wiki tatu zilizopita, machafuko yameongezeka kwa kasi kila kunapoteokea maandamano katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris, ambako kulitokea machafuko makubwa siku ya Jumamosi.

Kufuatia kuzuka kwa mgogoro uliosababishwa na waandamaji wanaopinga kuongezwa kwa kodi ya mafuta nchini Ufaransa, serikali imesema iko tayari kuachana moja kwa moja na hatua ya kupandisha kodi ya bidhaa hiyo kama hakutapatikana "ufumbuzi mzuri."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.