Pata taarifa kuu
UFARANSA-SIASA

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa ajiuzulu

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, hatimaye amekubali kujiuzulu kwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo Gérard Collomb. Hatua ambayo imewashangaza wengi nchini Ufaransa.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Gerard Collomb, Septemba 28, 2018.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Gerard Collomb, Septemba 28, 2018. ROMAIN LAFABREGUE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ufaransa amemtaka Waziri Mkuu Edouard Philippe kukaimu nafasi hiyo, ikulu ya Elysée imetangaza usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano wiki hii. Baraza la Mawaziri linatarajia kukutana Jumatano wiki hii ofisi ya rais imeongeza.

Uamuzi huu umewashangaza wengi, jambo ambalo halijawahi kutokea katika tangu rais Macron kuchukuwa madaraka.

Emmanuel Macron "amekubali kujiuzulu kwa Gérard Collomb na kumwomba Waziri Mkuu kukaimu nafasi hiyo kwa kusubiri uteuzi wa mrithi wake" katika Wizara ya Mambo ya Ndani, ikulu ya Elyséee imetangaza mapema Jumatano wiki hii.

Mapema Jumanne jioni, uvumi - ambao ulithibitishwa usiku- kuhusu hatua ya Waziri Mkuu kufuta ziara yake iliyokuwa imepangwa wiki hii nchini Afrika Kusini ilionekana kuwa suala la Gérard Collomb lilikuwa kipaumbele kwa serikali.

Kiongozi huyo nambari 2 wa serikali aliwasilisha kwa mara nyingine barua yake ya kujiuzulu kwa rais Macron Jumanne wiki hii, chini ya saa 24 baada ya rais kukataa ombi lake la kujiuzulu, akisema kuwa bado ana imani naye.

Awali Gérard Collomb alilithibitisha gazeti la Fgaro kuwa yuko tayari kujiuzulu.

Tayari maswali mengi yameibuka kuhusu hatua hiyo ya kujiuzulu ya Gérard Collomb

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.