Pata taarifa kuu
UGIRIKI-MAJANGA YA ASILI-USALAMA

Mkasa wa moto Ugiriki: Shughuli za uokoaji zaendelea

Kulingana na ripoti ya mwisho watu 74 wamefariki na 187 wamejeruhiwa kutokana na mkasa wa moto mkubwa uliozuka katika Jimbo la Athens na mashariki mwa Ugiriki.

Mati, karibu na Athens, Julai 24, 2018: mwanamke huyu anasikitika kumpoteza mbwa wake katika gari lake lililoteketea kwa moto.
Mati, karibu na Athens, Julai 24, 2018: mwanamke huyu anasikitika kumpoteza mbwa wake katika gari lake lililoteketea kwa moto. REUTERS/Costas Baltas
Matangazo ya kibiashara

Kutokana na upepo mkali, moto ulisambaa haraka, na hali hiyo ilisababisha kuongezeka kwa idadi ya waathirika. Siku tatu za maombolezo ya kitaifa zimetangazwa, na katika mikoa iliyoathirika, watu wameendelea kushikamana katika shughuli za uokoaji.

Nchi nyingi zimetoa msaada wao kwa Ugiriki ili kupambana na moto huo unaoharibu misitu karibu na mji mkuu. Nchi kadhaa za Ulaya, lakini pia nchi jirani kama Uturuki, Israeli au Jamhuri ya zamani ya Yugoslavia ya Makedonia zimetoa msaada wao kwa Ugiriki.

Takribani watu 74 wamethibitishwa kufariki lakini idadi ya watu ambao waliopotea bado haijajulikana.

Wakazi wanasema walilazimika kukimbilia baharini kujiokoa walipoona wamezingirwa na moto huo.

Mamlaka katika mji huo zina mashaka kuhusiana na chanzo cha moto huo na kwamba huenda umesababishwa makusudi.

''Nchi inapitia katika wakati mgumu sana. Mamia ya watu wamefariki na hili linamuumiza kila mmoja haswa kwa familia zilizopoteza wapendwa wao. Leo Ugiriki inaomboleza, na kwa kumbukumbu ya wale wote waliofariki tunatangaza siku tatu za maombolezo,'' alisema Tsipras.

Serikali ya Ugiriki inasema kuna uwezekano mkubwa watu wengi zaidi wakawa wamefariki katika kisa hicho ambacho kimeacha simanzi kwa nchi nzima.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.