Pata taarifa kuu
ICC-HAKI

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, yatimiza miaka 20 tangu kuundwa kwake

Leo ni miaka 20 imetimia tangu kuundwa kwa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC kupitia mkataba wa Roma. Ni siku ambayo imekuja wakati huu mahakama hiyo ikikabiliwaana ukosoaji mkubwa kutoka kwa wadau mbalimbali.

Makao makuu ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC.
Makao makuu ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC. Wikipédia
Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ya ICC ni mahakama ya kwanza ya kudumu ya kimataifa ilioundwa ili kuwafikisha mahakamani watu wanaohusika na uhalifu mkubwa ikiwa ni pamoja na uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya binadamu na mauaji ya kimbari, wakati mahakama za kitaifa zikiw ahazina uwezo wa kuhukumu. Mkataba huu ulikuwa umejadiliwa kwa karibu miaka mitatu, na ulipitishwa baada ya kikao kilichofanyika huko Roma Julai 17, 1998.

Miaka ishirini tangu kuundwa kwake ICC imechunguza kesi 26, nyingi zikiwa bado katika awamu ya majaribio, imetowa waranti 32 za kukamatwa, 15 zilitekelezwa huku ikiwa na wafungwa sita ambao wote wanazuiliwa. Ilichukua miaka 14 baada ya kupitishwa kwa Sheria ya Roma ili kuona mtuhumiwa wa kwanza wa ICC aakihukumiwa.

Thomas Lubanga, kiongozi wa wanamgambo wa Ituri ambaye alihukumiwa miaka 14 jela mwaka 2012 kwa kuwaajiri watoto jeshini. Ikiwa ni moja mwa tukio la mfano kwa mahakamani ambalo liliwapa wasiwasi viongozi wa makundi ya waasi. Wakati huo, kiongozi mmoja wa waasi nchini Tchad alishangazwa kuona Lubanga anakuhumiwa tu kwa kosa la kuwaajiri watoto jeshini.

Hata hivyo mahakama hiyo imeendelea kukosolewa na wataalamu wa maswala ya sheria ambao wanaonakuwa kuna makosa mengi ambayo yanafanyika lakini ICC imeshindwa kuyashiguhulikia.

Kwa hatuwa ya kwanza mahakama ya ICC ilianza kuchunguza makosa yanayotendeka barani Afrika ambapo awali ni mataifa yenyewe ya Afrika ndio yalitowa wito kwa ICC kuchunguza makosa.

Inaelezwa kuwa mataifa mengi ya Afrika yalisaini kwa pamoja kwenye mkataba huo wa Roma mataifa 34, huku Ulaya mataifa 25 na visiwa vya Caraibean na Amerika nchi 28 zikijiunga.

Wakati mahakama hiyo ilianza kuwashambulia viongozi kama vile Omar el Bachir wa Sudani, Uhuri Kenyatta wa kenya na naibu wake William Rutto, Umoja wa Afrika ulianza kulalama kuwa mahakama hiyo sasa yaonekana kuwa ni ya wazungu dhidi ya wa Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.