rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Ujerumani Uhispania Carles Puigdemont

Imechapishwa • Imehaririwa

Puigdemont kupelekwa Madrid kwa makosa ya ubadhirifu

media
Kiongozi wa zamani wa Catalonia Carles Puigdemont, Mei 15, 2018 Berlin. © AFP

Mahakama ya Ujerumani imeagiza Alhamisi wiki hii kiongozi wa zamani wa Catalonia Carles Puigdemont kupelekwa nchini Uhispania kwa makosa ya ubadhirifu.


Kwa upande mwengine mahakama hiyo imefutilia mbali kosa kubwa la uasi lililokua likimkabili Bw Puigdemont.

"Carles Upigdemont anaweza kupelekwa nchini Uhispania kwa makosa ya ubadhirifu, lakini kosa la uasi dhidi ya kiongozi huyo wa zamani wa Catalonia halikubaliki," mahakama ya Schleswig-Holstein imesema, na kuongeza kwamba mwendesha mashitaka ameruhusiwa kuanzisha utaratibu kwa kumkabidhi Carles Puigdemont kwa serikali ya Uhispnia.

Wakati huo huo ofisi ya mashitaka imesema kwamba "itaangalia kama itawezekana kutoa idhni ya kumkabidhi Bw Carles kwa serikali ya Uhispania kwa kosa la ubadhirifu."

Uamuzi wa mahakama ni pigo kubwa kwa serikali ya Uhispania ambayo imekua ikimshtumu Carles Puigdemont kosa la uasi na kuchochea machafuko, uhalifu unaoadhibiwa na kifungo cha miaka 30 jela nchini Uhspania.

Majaji pia wamefutilia mbali hoja ya Carles Puigdemont kwamba amefunguliwa mashitaka kwa sababu za kisiasana kwamba ombi la kutumwa nchini Uhispania linaweza kusitishwa.