rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Ufaransa

Imechapishwa • Imehaririwa

Polisi yadai kumuua kimakosa kijana mmoja Nante

media
Gari llikiteketea kwa moto huko Nantes, Julai 6, 2018, wakati machafukobaada ya kijana mmoja kuuawa kwa kupigwa risasi na polisi. Esther DELORD / AFP

Watu wanne wamekamatwa katika mji wa Nantes, nchini Ufaransa, ambapo majengo manane yaliharibiwa na magari 52 yalichomwa moto, ikiwa ni pamoja na lile la Meya.


Machafuko haya yameingia usiku wake wa watatu wa machafuko Alhamisi kuamkia Ijumaa wiki hii, baada ya mtu mmoja kuuawa kwa risasi Julai 3. Polisi imeendelea kunyooshwa kidole cha lawama kuhusiana na tukio hilo.

Katika mji wa Nantes, ofisi ya kampuni ya bia-PMU imeharibiwa kwa moto katika kata ya biashara ya Doulon. Majengo kadhaa ya serikali, ikiwa ni pamoja na shule ya ufundi ya Leonardo de Vinci na shule moja katika eneo la Bottière, kaskazini-mashariki mwa Nantes, nyumba ya ajira huko Malakoff na nyumba ya wakazikatika eneo la Bellevue zimechomwa moto.

Katika machafuko hayo, magari 52 yalichomwa moto, hasa hasa Bottière, Bellevue na katika maeneo ya kaskazini mwa Nantes. Gari la meya PS wa Nantes, Johanna Rolland ni miongoni mwa magari yaliyochomwa moto.

Watu wanne wamekamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi, ikiwa ni pamoja mtoto mwenye umri wa miaka14 ambaye alikuwa dumu la petroli. Hata hivyo hali ya utulivu ilirejea kwenye saa 6:00 asubuhi.

"Ukweli na haki"

Hakuna hasara iliyoripotiwa katika wilaya ya Breil, ambapo kijana mmoja aliliuawa kwa kupigwa risasi Jumanne, Julai 3 jioni na afisa polisi, na hivyo kusababisha kuzuka maandamano katika wilaya kadhaa za Nantes.

Afisa wa polisi aliyehusika na kifo hicho amezuiliwa kwa amri ya uongozi wa polisi kwa kusababisha kifo bila kukusudia.