rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Ufaransa

Imechapishwa • Imehaririwa

Mwizi sugu atoroka jela kwa Helikopta nchini Ufaransa

media
Mwizi sugu raia wa ufaransa Redoine Faid DW

Mwizi sugu ambaye wakati mmoja alikuwa anatafutwa sana nchini Ufaransa, ametoroka jela na kutoweka akiwa ndani ya helikopta jijini Paris.


Ripoti zinasema kuwa, Redoine Faid, mwenye umri wa miaka 46 akisaidiwa na watu wengine waliokuwa wamejihami kwa silaha, walifunga lango la jela alimokuwa anazuiwa na baadaye kutoroka.

Hata hivyo, helikopta hiyo imepatikana Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo wakati huu, polisi waliendelea na msako wa kumtafuta mwizi huyo.

Hii ni mara ya pili kwa Faid kutoroka jela.Mwaka 2013, alifanikiwa kutoka lakini akamatwa baada ya wiki sita.

Amefungwa jela miaka 25, baada ya kupatikana na kosa la wizi wa mabavu mwaka 2010 na kusababisha kifo cha polisi mmoja.