Pata taarifa kuu
EU-WAKIMBIZI-USALAMA

Umoja wa Ulaya kujadili suala la wahamiaji

Nchi ishirini na nane za Ulaya zinakutana Alhamisi na Ijumaa wiki hii huko Brussels, Ubelgiji, kujadili masuala mbamlimbali, lakini suala linalopewa kipaumbele ni lile la wahamiaji wanaoingia barani Ulaya. Nchi wanachama zimegawanyika kuhusu suala hili.

Hatima ya wahamiaji waliosafirishwa na Aquarius (hapa wakiwasili Valencia Juni 17, 2018) imepelekea viongozi wa nchi za Ulaya kukutana ilikujadili kuhusu suala la wahamiaji wanaoingia Ulaya.
Hatima ya wahamiaji waliosafirishwa na Aquarius (hapa wakiwasili Valencia Juni 17, 2018) imepelekea viongozi wa nchi za Ulaya kukutana ilikujadili kuhusu suala la wahamiaji wanaoingia Ulaya. Kenny Karpov/SOS Mediterranee/Handout via Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mapendekezo kadhaa yametolewa ili kudhibiti wimbi la wahamiaji hata moja ambalo wamekubaliana.

Suala wahamiaji unaendelea kuzisakama nchi za Ulaya, na kwa sasa inaonekana kuwa mjadala kuhusu suala hilo utachukua muda mrefu katika mkutano huo," tayari ameangaza Donald Tusk saa chache baada ya ufunguzi wa mkutano huo mjini Brussels. Rais wa Baraza la Ulaya Donald Tusk ameonya kuwa mgawanyiko unaotokana na kukabiliana na wimbi la wahamiaji ni ishara tosha ya udhaifu wa Umoja wa Ulaya na kuchochea hali ya sintofahamu dhidi ya wageni. Hakun aimani yoyote kuwa mkutano huu utazaa matunda yoyote, kutokana na kuwa viongozi mbalimbali wa umoja huo wanatofautiana kuhusu suala hilo.

Baada ya kukataa kufungua bandari zake kwa meli mbili za shirika la kihisani linalohusika na kuwasafirisha wahamiaji wanaookolewa baharini, Italia inatarajia kutoa mfululizo wa mapendekezo, ikiwa ni pamoja na kuundwa kwa vituo vya ulinzi katika nchi wanakopita wahamiaji. Kwa upande wao, Ufaransa na Uhispania wanasisitiza kufunguliwa kwa vituo vilivyofungwa barani Ulaya karibu na maeneo ambapo wahamiaji wamekua wakiwasili na hapo ndipo maombi kuhusu kupewa hifadhi ya kimbizi yatathminiwa.

Kinyume na nchi za Ulaya ya Kati, Austria inapendekeza kuanzishwa kwa vituo vya mapokezi kwa wahamiaji nje ya nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya. Albania imetajwa miongoni mwa nchi ambako kunaweza kujengwa vituo hivi, lakini tayari nchi imefutilia mbali pendekezo hilo.

Katika barua kwa viongozi wa Muungano kabla ya mkutano huo, rais wa Baraza la Ulaya amewaomba kuidhinisha utekelezaji wa "utaratibu wa kuwapokea wahamiaji au wakimbizi nje ya Ulaya." Hata hivyo, nchi ishirini na nane, wanachama wa Umoja wa Ulaya, wanaonekana kukubaliana juu ya hatua moja tu: udhibiti wa mipaka ya nje ya eneo la Schengen uimarishwe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.