Pata taarifa kuu
UFARANSA-VATICAN-USHIRIKIANO

Emmanuel Macron azuru Vatican

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amezuru Jumanne wiki hii Vatican na kukutana kwa mara ya kwanza ana kwa ana na kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis.

Papa Francis amempokea Rais wa Ufaransa katika mazungumzo yao binafsi Jumanne, Juni 26, 2018.
Papa Francis amempokea Rais wa Ufaransa katika mazungumzo yao binafsi Jumanne, Juni 26, 2018. Alessandra Tarantino/Pool via Reuters
Matangazo ya kibiashara

Hii ni ziara yake ya kwanza katika mji huo mtakatifu kwa waumini wa Kanisa Katoliki tangu aingie madarakani. Atatumia fursa hii kupokea tuzo kutoka kanisa la Mtakatifu John Lateran, tuzo la kihistoria la heshima. Lakini atakutana hasa na Papa Francis katika mazungumzo binafsi.

Huu ni mkutano wa kwanza kati ya Papa Francis na Emmanuel Macron. Wawili hao wamezungumza kwa muda wa saa moja na nusu, wakianza kwa kujitambulisha kwa kila mmoja.

Zaidi ya mwaka mmoja uliopita, Papa Francis aliulizwa kuhusu wagombea wakati wa kampeni za uchaguzi wa urais nchini Ufaransa, alisema kuhusu Emmanuel Macron: "Sijui wapi anatoka".

Tangu wakati huo, rais wa Ufaransa na kiongozi wa Kanisa Katoliki wamezungumza mara moja kwenye simu wakati rais Macron alimpia simu Papa Francis akimshukuru kwa kuhusika kwake katika suala la tabia nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.