Pata taarifa kuu
EU-UNHCR-WAKIMBIZI

UNHCR yaomba Ulaya kuharakisha taratibu za mapokezi kwa wakimbizi

Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR), Filippo Grandi, ameomba nchi za Ulaya kuharakisha taratibu za kuondoka kwa wakimbizi katika nchi wanakopita ambao waliamua kuwapokea.

Filippo Grandi , Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi. UNHCR.
Filippo Grandi , Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi. UNHCR. REUTERS/Denis Balibouse
Matangazo ya kibiashara

"Tumekuwa na idadi kubwa ya makazi ya wakimbizi yanayotolewa na" nchi nyingi za Ulaya ", lakini" kile kinachotia wasiwasi ni utekelezaji wa zoezi hilo ambao unakwenda kwa mwendo wa kinyonga, "amesema Filippo Grandi wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Niamey wakati wa maadhimisho wa Siku ya Wakimbizi Duniani.

Grandi aliwasili Niger Jumanne wiki hii kutoka Libya, ambapo aliyaleta makundi ya wakimbizi waliokua wakizuiliwa nchini humo.

"Ninatarajia nchi za kuwapokea (kutoka Ulaya) kuwa taratibu zitakua za haraka, na zenye ufanisi.

Mchi za Ulaya naelezea "haja ya kuimarisha uangalifu katika pwani ya Libya" na "ni haki yao," lakini wakati huo huo, watu wanajikuta katika hali ngumu sana nchini Libya," ameonya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.