rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Ubelgiji Jean-Pierre Bemba DRC

Imechapishwa • Imehaririwa

Ubelgiji yakubali kumpa makaazi Bemba

media
Jean-Pierre Bemba REUTERS/Michael Kooren/File Photo

Ubelgiji imesema iko tayari kumpokea na kumpa makaazi Jean Pierre Bemba, aliyekuwa Makamu wa rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, baada ya Mahakama ya Kimataifa ya ICC, kumwachilia huru wiki hii.


Waziri wa Mambo ya nje wa nchi hiyo Didier Reynders amesema utaratibu unaendelea,ili kumruhusu Bemba kuungana na familia yake inayoishi katika taifa hilo la bara Ulaya.

Bemba, ameomba kuishi nchini Ubelgiji kwa muda wa miezi mitatu na tayari ameomba kibali.

Haijafamika iwapo atarejea nchini DRC na labda kuwania urais mwezi Desemba.

Bonyeza hapa kusoma zaidi kuhusu Bemba:-