rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
  • Mafuriko yameua watu kumi na nane Iran (idara ya hali ya Dharura)

Uingereza

Imechapishwa • Imehaririwa

Harusi ya Kifalme na kifahari yafanyika Uingereza

media
Meghan na Mwanamfalme Harry wakati wakifunga ndoa Mei 19 2018 (Foto: Reuters)

Nchini Uingereza, kumekuwa na harusi ya kifalme na ya kifahari kati ya Mwanamfalme Harry na Mmarekani Meghan Markle.


Wawili hao ni rasmi sasa kuwa ni  Mume na Mke, baada ya kufunga ndoa katika Kanisa la Angilika la Mtakatifu George katika eneo la Windsor.

Wawili hao walishangiliwa na kusalimiwa na maelfu ya watu waliokuwa wamejipanga pembezoni mwa barabarani kuwaona baada ya kutoka Kanisani.

Miongoni mwa wageni washuhuri walikuwa ni pamoja na Malkia Elizabeth wa pili miongoni mwa wengine kutoka Uingereza na Marekani.

Mwanamfalme Harry, yupo katika orodha ya kuwa miongoni mwa watu wanaoweza kuwa Wafalme wa Uingereza katika siku zijazo.