rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Ufaransa Ajira Emmanuel Macron Edouard Philippe

Imechapishwa • Imehaririwa

Edouard Philippe kukutana na vyama vya wafanyakazi wa reli

media
Watumishi wa umma wakiandamana dhidi ya mageuzi ya SNCF, tarehe 19 Aprili 2018, huko Nantes. REUTERS/Stephane Mahe

Waziri Mkuu wa Ufaransa anatarajia kukutana Jumatatu hii, Mei 7, na vyama vya wafanyakazi vya SNCF. Shirikisho nne za reli na viongozi wa vyama vikuu vya wafanyakazi watapokelewa kila mmoja baada ya mwengine katika ofisi ya Waziri Mkuu Edouard Philippe, wakati ambapo Jumapili maandamano yalikua yaliingia siku yake ya nane.


Haijafahamika iwapo mikutano hii itapatia ufumbuzi mgogoro huu. Bw Philippe anasema "yuko wazi kwa mazungumzo lakini yuko makini".

"Nitafurahi wakiridhishwa". Amesema Edouard Philippe wakati ataposikia vyama vya wafanyakazi vikipiga kelele "ushindi" baada ya mikutano hiyo. Mazungumzo kati ya Waziri Mkuu Edouard Philippe na viongozi wa vyama hivyo yatajikita kwenye masuala nyeti

Mipaka tayari imewekwa. "Tutazungumza bila kuingilia yaliyopigiwa kura katika Bunge," washirika wa karibu wa Edouard Philippe wamesema. Hakuna swali la kurudi kwenye mageuzi ya sheria ya wafanyakazi wa reli au ufunguzi kwa ushindani.

Kwa upande mwingine, mlango unaendelea kuwa wazi kwa "kujadili madeni" ofisi ya waziri Mkuu imesema katika taarifa yake.

Siku ya Jumamosi maelfu ya watu waliandamana jijini Paris kupinga mabadiliko yanayofanywa na serikali ya rais Emmnuel Macron.

Maandamano haya yalikuja wakati rais Macron mwenye umri wa miaka 40, akidhimisha mwaka mmoja madarakani tangu kuchaguliwa kuwa rais wa taifa hilo la bara Ulaya.

Polisi wa kupambana na ghasia wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 2,000 walionekana jijini Paris, huku maandamano mengine yakifanyika katika miji ya Kusini ya Toulouse na Bordeaux .

Serikali ilisema ililazimika kutuma maelfu ya polisi barabarani kwa hofu ya kutokea kwa machafuko na uharibifu wa mali kama ilivyoshuhudiwa wakati wa sikukuu ya wafanyakazi tarehe 1 mwezi huu.

Siku za hivi karibuni kumeshuhudiwa ongezeko la maandamano nchini Ufaransa kupinga sera mpya za rais Macron kwa watumishi wa umma ikiwemo sekta ya elimu na usafiri hasa wanaofanya kazi katika shirika la reli.

Rais Macron ameendelea kusisitiza kuwa ataendelea na mabadiliko hayo, kwa lengo la kuimarisha uchumi wa taifa hilo, licha ya pingamizi kutoka kwa wafanyakazi wa umma.