rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Ufaransa Emmanuel Macron

Imechapishwa • Imehaririwa

May Day: Watu 200 wakamatwa baada ya vurugu Ufaransa

media
Wanaharakati 1,200 kutoka kundi la Bloc Black walikusanyika mbele ya msafara wakati wa gwaride la Mei 1 huko Paris. REUTERS/Philippe Wojazer

Polisi jijini Paris nchini wanasema waliwakamata waandamanaji karibu 200 walioharaibu magari ya watu na kuchoma maduka wakati wakiandamana wakati wa siku ya kimataifa ya wafanyakazi.


Polisi inasema ilihesabu watu 20,000 na wengine 14,500 waliokua mbali na msafara wa shirikisho la vyama hivyo, ikiwa ni pamoja na wanachama 1,200 wa kundi lenye msimamo mkali la "Black Blocks", waliohusika na vurugu kando ya maadhimisho hayo. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amelaani vurugu hizo akisema zilichochewa na kundi dogo la watu ambao walipoteza maadili.

Shirikisho la vyama wafanyakazi CGT nchini Ufaransa limesema kuwa katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wafanyakazi uliwakusanya watu 55,000 mjini Paris pekee dhidi ya 80,000 mwaka jana.

Makabiliano yalianza kati ya polisi na wanaharakati wa kundi la"Black Blocs" karibu na kituo cha magari cha Austerlitz huko Paris, Mei 1. St├ęphane Lagarde/RFI

Waandamanaji hao walikuwa wakiandamana kupinga mabadiliko ya kazi yaliyofanywa na serikali ya rais Emmanuel Macron.

Polisi wanasema, watu zadi ya 1200 waliokuwa wamejifunika nyusa zao, walivamia maandamano ya amani yaliyokuwa yameandaliwa na vyama vya wafanyakazi nchini humo.

Mwanaharakati wa kundi la Bloc Black akipita mbele ya gari likiwaka moto karibu na ofisi za kampuni ya Renault iliyoshambuliwa huko Paris. REUTERS/Christian Hartmann