Pata taarifa kuu
UINGEREZA-SIASA-UHAMIAJI

Theresa May ateua Waziri mpya wa mambo ya ndani

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amemteua Sajid Javid kama Waziri wa Mambo ya Ndani, akichukua nafasi ya Amber Rudd, ambaye alijiuzulu siku ya Jumapili, kufuatia kashfa ya "Windrush".

Sajid Javid, Waziri mpya wa mambo ya Ndani wa Uingereza.
Sajid Javid, Waziri mpya wa mambo ya Ndani wa Uingereza. REUTERS/Toby Melville
Matangazo ya kibiashara

Kashfa hii inahusiana na matumizi mabaya ya mafaili ya maelfu ya wafanyakazi kutoka West Indies kati ya mwaka 1948 na 1971, ambapo aliwataja watu hao kama "wahamiaji haramu". Sajid Javid, mwenye umri wa miaka 48, ambaye alikua akishikilia nafasi kwenye uongozi wa Deutsche Bank, kabla alikuwa katibu wa Makazi.

Sajid Javid ni Katibu Waziri wa Mambo ya Ndani katika Ofisi ya waziri mkuu kutoka kabila la watu wachache. Sajid Javid ni mwana wa dereva wa basi kutoka Pakistani ambaye aliwasili nchini Uingereza katika miaka ya 196. Alizungumzia mara nyingi kuhusu kashfa ya wahamiaji wa Caribbean kutoka "kizazi cha Windrush".

Theresa Maya ameendelea kukosolewa na wapinzani wake wakati huo joto la kisiasa likiendelea kupanda kufuatia uchaguzi wa mitaa ambao utafanyika Alhamisi wiki hii na itakuwa mtihani kwa serikali yake inayokabiliwa na visa vya kujiuzulu kwa maafisa kadhaa, huku majadiliano kati ya London na Brussels yanaanza tena kuhusu kujiondoa kwa taifa hilo katika Umoja wa Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.