rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Urusi Ujerumani

Imechapishwa • Imehaririwa

Shambulio la kimtandao: Ujerumani yashtumu Urusi

media
Vita vya mtandao yahoo.fr

Serikali ya Ujerumani imebaini kwamba shambulio dhidi ya Wizara ya Mambo ya Nje mnamo mwezi Desemba mwaka jana liliendeshwa na Urusi, Waziri wake wa Mambo ya Kigeni amesema.


Heiko Maas, ambaye alizungumza kwenye kituo cha televisheni cha ZDF, aliorodhesha kile alichokiita vitendo vya matatizo ya Moscow, ikiwa ni pamoja na ukosefu wa maendeleo katika kusitisha mapigano.

Mashariki mwa Ukraine, shambulio la gesi yenye sumu nchini Uingereza, msaada wa Moscow kwa serikali ya Syria, majaribio ya kushawishi uchaguzi katika nchi kadhaa za Magharibi na shambulio kubwa la kimkakati la kimtandao.

"Tulikumbwa na shambulio dhidi ya Wizara ya Mambo ya Nje ambapo tunadhani kwamba shambulio hilo lilitoka Urusi," Waziri wa mambo ya Nje wa Ujerumani Heiko Maas amesema.

"Hatuwezi tu kutumaini kwamba yote haya yafanyike ... na nadhani sio busara tu, lakini ni muhimu kusisitiza kwamba hatuoni kabisa yote haya kama ni michango yenye kujenga, " Waziri Maas ameongeza.

Mpaka sasa Urusi haijazungumza chochote baada ya tuhuma hizo.