rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Ufaransa Nicolas Sarkozy Libya Muammar Gaddafi

Imechapishwa • Imehaririwa

Ufaransa: Nicolas Sarkozy kupanda kizimbani kujibu tuhuma za rushwa

media
Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy ambaye sasa atashtakiwa kwa makosa ya rushwa nchini mwake. 21.01.2018. REUTERS/Gonzalo Fuentes

Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy ameagizwa kupandishwa kizimbani kujibu mashtaka ya rushwa na kumshawishi jaji mmoja kuingilia taarifa za uchunguzi dhidi yake.


Waendesha mashataka pia wamependekeza wakili wa Sarkozy Thierry Herzog na jaji wa zamani Gilbert Azibert nao washtakiwe katika kesi ya mwaka 2014.

Ikiwa kesi yao itathibitishwa, itakuwa ni kesi ya pili inayomkabili kiongozi huyo ambaye anatarajiwa kushtakiwa kwa makosa ya kupokea fedha kutoka kwa rais wa zamani wa Libya Marehamu Kanali Muamar Gaddafi, fedha zilizotumika kufadhili kampeni zake za urais mwaka 2012.

Hata hivyo inatarajiwa kuwa Sarkozy huenda akakata rufaa kupinga uamuzi huo.

Kiongozi huyu mwenye umri wa miaka 63 pia anashtakiwa kwa makosa ya kupokea fedha kutoka kwa kiongozi wa zamani wa Libya Muamar Gaddafi, tuhuma ambazo ameendelea kukanusha.

Kesi ya ushawishi inahusu mawasiliano kati ya wakili wake na jaji Azibert mazungumzo ambayo yalirekodiwa na wachunguzi ambao walikuwa wanaangalia ikiwa Sarkozy alikubali malipo kutoka kwa kampuni ua L’Oreal heiress Liliane Bettencourt.

Hata hivyo alisafishwa kutokana na kashfa ya Bettencourt mwaka 2013 lakini mazungumzo yaliyorekodiwa yanaashiria kuwa alijaribu kumueleza jaji Azebert kumpa taarifa za kesi yake kwa kumuahidi kazi mjini Monaco.

Mwaka 2014 Sarkozy alikuwa rais wa kwanza wa Ufaransa kushikiliwa na polisi wakati wa uchunguzi wa awali.

Hata hivyo sio rais wa kwanza wa zamani kushtakiwa kwa makosa ya rushwa, mtangulizi wake Jacques Chirac alihukumiwa miaka miwili mwaka 2011 kwa makosa ya matumizi mabaya ya fedha za uma wakati akiwa Meya wa jiji la Paris.

Sarkozy anasisitiza kuwa kesi dhidi yake zimechochewa kisiasa na kwamba hana hatia dhidi ya tuhuma zinazomkabili.