rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Ufaransa

Imechapishwa • Imehaririwa

Wanajeshi wa Ufaransa wanusurika katika shambulio

media
Wanajeshi wakilinda lango la kuingia kwenye kambi namba 7 ya CBA de Reynies Varces-Allieres-et-Risset. Machi 29, 2018.ng nearby. JEAN-PIERRE CLATOT/AFP

Polisi nchini Ufaransa inawashikilia watu wawili baada ya kundi la wanajeshi kunusirika kugongwa na gari wakati wakifanya mazoezi jirani na kambi yao ya jeshi kusini magharibi mwa Ufaransa.


Wanajeshi kutoka kikosi cha 7 walifanikiwa kulikwepa gari lililokuwa likielekea kuwagonga kwenye eneo la Varces-Allieres-et-Risset.

Dereva wa gari hilo anadaiwa kutamka maneno ya kiarabu kwa wanajeshi hao kabla ya kujaribu kuwagonga na kisha kuendelea na safari yake akiwa katika gari aina ya Peugeot 208 ikiwa na namba bandia.

Taarifa zinasema kuwa kwenye gari hilo alikuwemo pia mwanamke mmoja na hakuna alijeruhiwa.

Polisi baadae iliandika kwenye mtandao wake wa kijamii kuwa wanamshikilia mtu mmoja kwenye soka la Grenoble baada ya kuendesha msako.

Katika taarifa tofauti polisi wamedai pia kumshikilia mmiliki wa gari kwenye eneo la Échirolles mji ulioko kusini mwa Grenoble.

Mwenseha mashataka mjini Grenoble amesema tukio hilo halichunguzwi kama tukio la kigaidi.

Tukio hili limetekelezwa siku chache tu tangu kuuawa kwa watu wanne katika tukio la utejkaji kwenye duka moja la jumla kusini magharibi mwa mji wa Trébes.

Mtu mwenye silaha Radouane Lakdim alianza shambulio lake Machi 23 jirani na mji wa Carcassonne kwa kuwafyatulia risasi maofisa wa polisi ambao walikuwa wkaifanya mazoezi na kumjeruhi afisa mmoja.

Polisi walovamia duka la Super U baada ya Lakdim kushikilia watu kadhaa mateka na kupigwa risasi kichwani.

Mchumba wake mwenye umri wa miaka 18 ameshtakiwa kwa kuwa sehemu ya ushiriki wa mtandao wa kigaidi.