Pata taarifa kuu
EU-MAREKANI-URUSI

Nchi za Ulaya kuwafukuza wanadiplomasia zaidi wa Urusi

Jumuiya ya nchi za Kujihami za Magharibi NATO juma hili imeungana na mataifa mengine 25 duniani kuwafurusha wanadipolomasia wa Urusi katika kile kinachoonekana ni kujibu kile wanachosema ni hatua ya Serikali ya Moscow kutumia sumu inayoathiri mishipa ya fahamu dhidi ya jasusi wake wa zamani jijini London.

Mkuu wa sera za kigeni wa umoja wa Ulaya Federica Mogherini akizungumza akiwa kwenye makao makuu ya NATO.
Mkuu wa sera za kigeni wa umoja wa Ulaya Federica Mogherini akizungumza akiwa kwenye makao makuu ya NATO. ©THIERRY CHARLIER / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imeelezwana nchi ya Uingereza kama ukurasa mpya wa namna mataifa ya magharibi yatashirikiana na Urusi.

NATO imewafukuza wanadiplomasia 7 wa Urusi na kukataa kutoa vibali kwa wengine watatu na kufanya idadi ya watu wanaotajwa kuwa wapelelezo wa Urusi waliofukuzwa kufikia 150 wakiwemo wale 23 waliofukuzwa na Uingereza.

“Hatua hii itatuma ujumbe wa wazo kwa Urusi kuwa kuna gharama na hasara ya vitendo vyao ambavyo havikubaliki,” amesema katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg akiwa mjini Brussels.

Katika kile kinachoonekana sio kitu cha kawaida, nchi 25 zimeungana na Uingereza kuchukua hatua kutokana na tukio la Machi 4 ambapo jasusi wa zamani wa Urusi Sergei Skripal na mwanae wa kike Julia waliwekewa sumu kwenye mji wa Salisbury.

Serikali ya London na washirika wake wanailaumu Serikali ya Moscow kwa kile wanachosema utawala huo kutumia sumu ya Novichok ambayo inadaiwa kutumiwa na Urusi kushambulia raia wake waliokimbia.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza Boris Johnson amesema kufukuzwa kwa wanadiplomasia hao ni pigo kwa Urusi ambayo itachukua muda mrefu kujenga idara yake ya ujasusi.

Skripal ambaye ni mwanajeshi na mpelelezi wa zamani alifungwa na Urusi kwa kutoa taarifa kwa mataifa ya Ulaya kuhusu nchi yake, alikimbilia Uingereza mwaka 2010 kwa mabadilishano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.