Pata taarifa kuu
UFARANSA

Wafanyakazi wa shirika la ndege la Ufaransa wafanya mgomo

Wafanyakazi wa shirika la ndege la Ufaransa “Air France” wamefanya mgomo Ijumaa ya wiki hii na kusababisha kufutwa kwa zaidi ya robo tatu ya safari za shirika hilo wakati huu shirikisho la wafanyakazi nchini humo likijadili kufanya maandamano zaidi dhidi ya Serikali ya rais Emmanuel Macron.

Baadhi ya ndege za shirika la Air France zikiwa zimepaki.
Baadhi ya ndege za shirika la Air France zikiwa zimepaki. REUTERS/Charles Platiau
Matangazo ya kibiashara

Marubani, wafanyakazi wa ndani ya ndege na wale wa kawaida waliungana kwenye mgomo wa shirika hilo kushinikiza nyongeza ya asilimia 6.0 ya mshahara baada ya shirika hilo kurekodi faida katika mwaka 2017 kutokana na mabadiliko iliyoyafanya.

Mgomo huu ni tofauti na ule mkubwa ambao ni wazi utakuwa mvutano mkubwa kati ya Serikali ya rais Macron, wafanyabiashara pamoja na mashirikisho ya wafanyakazi ambayo yanapinga mabadiliko anayoyafanya.

Zaidi ya madereva laki tatu wa magari moshi, walimu, na wafanyakazi wa uma wameungana katika mgomo na maandamano ya nchi nzima siku ya Alhamisi, katika kile kinachosemwa ni hatua ya kwanza ya mfululizo wa maandamano.

Shirikisho la wafanyakazi la CGT ambao ni kubwa zaidi kwenye sekta ya uma, limeitisha mgomo mwingine wa nchi nzima April 19 na kuandaa mgomo mwingine wa wafanyakazi wanaokusanya taka.

Kumetokea mgawanyiko ikiwa mgomo wa Alhamisi ya wiki hii umetuma ujumbe kwa rais Macron, huku baadhi wakisema uliungwa mkono na watu wachache.

Hata hivyo wananchi wengi wanaunga mkono mabadiliko yaliyofanywa na rais Macron kuondoa upendelea kazini na wakati wa kuajiriwa ambapo kwenye sekta ya usafiri wa reli wafanyakazi wake wanamikataba ya maisha.

Macron pia ameahidi kupunguza ajira laki moja na elfu 20 ikiwa ni zaidi ya ajira milioni tano, akilenga makampuni kuajirti watu wenye vigezo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.