Pata taarifa kuu
UFARANSA

Ufaransa: Watu 3 wamekufa mjini Trebes, mtekaji apigwa risasi

Watu watatu wamekufa na wengine kadhaa wamejeruhiwa baada ya mtu mwenye silaha aliyedai kuwa mfuasi wa kundi la Islamic State kifaytua risasi na kuwateka watu kwenye duka moja la jumla kusini mwa nchi ya Ufaransa.

Polisi wa kupambana na ugaidi wakiwa nje ya duka la jumla la Super U kwenye mji wa Trebes ambako mtu mwenye silaha anawashikilia mateka watu kadhaa. 23 Machi 2018.
Polisi wa kupambana na ugaidi wakiwa nje ya duka la jumla la Super U kwenye mji wa Trebes ambako mtu mwenye silaha anawashikilia mateka watu kadhaa. 23 Machi 2018. LA VIE A TREBES/via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Taarifa zinasema kuwa tayari polisi wametekeleza shambulio na kufanikiwa kumuua mtekaji.

Vyombo ya usalama vinasema vimemtambua mtuhimiwa huyo kuwa mwenye asili ya Morocco ambaye alishakuwa chini ya uangalizi kama mmoja watu wenye ufuasi na makundi ya kijihadi.

Polisi wameendelea kujadiliana na mtuhumiwa huyo ambaye jina lake halijafahamika na ambaye ameendelea kujifungia kwenye duka la Super U kwenye mji wa Trebes baada ya kuvamia hapo majira ya asubuhi.

Mmoja wa mashuhuda amesema kuwa mshambuliaji huyo alijihami kwa visu, bunduki na mabomu na alikuwa akitamka maneni “Allahu Akbar” kabla ya kuingia kwenye duka hilo la jumla.

Watoa taarifa zaidi waliokaribu na timu ya uchunguzi wanasema kwa sasa wamefanikiwa kumtambua mshambuliaji kuwa mwenye asili ya Morocco.

Duka la jumla la Super U kwenye mji wa Trebes
Duka la jumla la Super U kwenye mji wa Trebes скриншот google maps

Polisi wanasema “wafanyakazi wengi wa duka hilo walifanikiwa kutoka sambamba na wateja lakini sio wote.”

Taarifa zaidi zinasema kwa sasa mtaalamu wa majadiliano tayari amefanikiwa kuwasiliana na mtekaji kuangalia uwezekano wa kumshawishi awaachie mateka.

Mkuu wa polisi kwenye mji wa Trebes Jean-Valery Lettermann amethibitisha vifo vya watu wawili, mmoja akiwa na polisi aliyepigwa risasi wakati mshambuliaji akiwa nyumbani na mwingine ni mteja anayedaiwa kupigwa risasi ya kichwa.

Waziri mkuu wa Ufaransa Edouard Philippe amesema tukio hili wanalitazama kama tukio la kigaidi na kwamba polisi aliyejeruhiwa wakati akiwa kwenye mazoezi ya kukimbia na wenzake hali yake inaendelea vizuri na hayuko kwenye hatari.

Polisi wanasema walilifuatilia gari la mtekaji kutoka kwenye kitongoji cha Carcassonne na baade kuligundua gari hilo limepakiwa kwenye eneo la duka hilo.

Taarifa zimeongeza kuwa mtu watatu amepatikana akiwa amekufa na mwili wake kupatikana ukiwa umetupwa kwenye mtaro ambapo taarifa zinadai kuwa huenda walikuwa ni wamiliki wa gari lilitekwa na mtuhumiwa, mmoja kati ya abiria anaripotiwa kuwa kwenye hali mbaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.