Pata taarifa kuu
URUSI-PUTIN

Rais Putin achaguliwa kwa kishindo katika uchaguzi uliokosolewa na upinzani

Rais wa Urusi Vladmir Putin anajiandaa kuongoza taifa hilo kwa miaka sita mingine baada ya kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu wa rais ambao hadi sasa ni washirika wake wa karibu ndio waliompongeza wakati huu uhusiano kati ya nchi yake na mataifa ya magharibi ukisuasua.

Rais wa Urusi Vladmir Putin ambaye amechaguliwa tena kuongoza nchi yake kwa miaka 6 mingine.
Rais wa Urusi Vladmir Putin ambaye amechaguliwa tena kuongoza nchi yake kwa miaka 6 mingine. Alexander Zemlianichenko/POOL via Reuters
Matangazo ya kibiashara

Rais Putin ambaye ameitawala Urusi kwa karibu miongo miwili, amepata ushindi wake wa kwanza mkubwa wa asilimia 76.67 ya kura zote lakini akakanusha pia taarifa kwamba amepanga kuwa rais wa kudumu.

Upinzani unasema kuwa matokeo hayo yametengenezwa, ukidai kuwa kuna masanduku ambayo kura ziliwekwa kabla pamoja na matukio mengine ya ukiukwaji wa sheria za uchaguzi.

Awali utawala wa Moscow ulikuwa umehamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi la upigaji kura katika kile kilichoonekana ni kujaribu kuufanya uchaguzi huo uwe wa kuaminika.

Rais Putin ambaye sasa ataongeza muda wa utawala wake hadi mwaka 2024 tayari ni kiongozi aliyeoongoza taifa hilo kwa muda mrefu zaidi tangu kumalizika kwa utawala wa Stalin.

"Nisikilizeni. Inaonekana kile unachosema ni kama utani kwangu," alisema rais Putin wakati akisisitiza kuwa hana mpango wa kuendelea kusalia madarakani hata baada ya kumaliza mihula yake.

Kiongozi huyo alishindani na wagombea wengine saba kwenye kinyang'anyiro hicho lakini wakosoaji wake wakubwa Alexei Navalny alizuiwa kushiriki uchaguzi huo kwa sababu za kisheria.

Akizungumza baada ya matokeo haya rais Putin amesema ameona namna wananchi wake walivyo na imani kwa utawala wake na kuamua kumpa muhula mwingine kuongoza taifa hilo.

Idadi ya watu waliojitokeza kupoiga kura inaelezwa kuwa ni zaidi ya asilimia 67.

Mashindano ya upigaji Selfie, utoaji wa zawadi, chakula na michezo ya watoto iliwekwa kwenye vituo vya kupigia kwa lengo la kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa uwingi.

Hata hivyo taarifa zimesema kuwa wafanyakazi wa uma na wale wa sekta binafsi waliripotiwa kushinikizwa kupiga kura kwenye uchaguzi huo.

Kwa mujibu wa tume ya uchaguzi wakati huu asilimia 99.8 ya kura zote zikiwa zimehesabiwa, rais Putin anaongoza kwa asiliamia 76.67 ya kura zotem akimuacha kwa mbali sana mpinzani wake wa chama cha Communist Pavel Grudinin ambaye amepata asilimia 11.79.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.