rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Israeli Jean Yves Ledrian Palestina

Imechapishwa • Imehaririwa

Mfanyakazi wa ubalozi wa Ufaransa Israel mbaroni kwa kusafirisha silaha Gaza

media
Wanajeshi wa Israel wakiwa kwenye eneo la Gaza REUTERS/Amir Cohen

Mfanyakazi mmoja wa ubalozi wa Ufaransa nchini Israel amefunguliwa mashtaka kwa tuhuma za kutumia gari la ofisi kusafirisha mamia ya silaha kutoka kwenye ukanda wa Gaza kwenda ukingo wa Magharibi.


Maofisa usalama wa Israel wamesema kuwa wamebaini mfanyakazi huyo kutoka ubalozi wa Jerusalem alikuwa akifanya kazi hiyo bila ya wasimamizi wake kujua na kwamba uhusiano wa nchi hizo mbili haujaathirika.

Kesi hii ambayo Israel inasema ni ya kipekee imefunguliwa ikiwa ni juma moja tu limesalia kabla ya kufanyika kwa ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian ambaye hatoepuka maswali kuhusu tukio la mfanyakazi wake.

Mfanyakazi huyo aliyekamatwa akiwa sambamba na raia kadhaa wa Palestina wanatuhumiwa kujihusisha na kushirikiana na mtandao wa uuzaji silaha.

Inadaiwa kuwa raia huyo Romain Franck mwenye umri wa miaka 23, anadaiwa kutumia kinga ya kidiplomasia ambayo magari ya ubalozi huwa hayakaguliwi mara kwa mara, kusafirisha silaha hizo kwa makundi ya wapiganaji wa Kipalestina.

Taarifa ya shirika la udhibiti wa silaha nchini Israel Shin, imesema kuwa mfanyakazi huyo kwa nyakati tofauti katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita alitumia gari ya ubalozi wa Ufaransa kukwepa vituo vya ukaguzi kwenye maeneo ya mipaka.

Shin inasema mfanyakazi huyo alisafirisha silaha hizo kwa zaidi ya mara sita waliwasilishwa mahakamani Jumatatu ya wiki hii.

Jumla ya watuhumiwa wengine 9 wamekamatwa na sita kati yao ni miongoni mwa waliopandishwa kizimbani.