Pata taarifa kuu
MAREKANI-UINGEREZA-IS-USALAMA

Marekani na Uingereza wajadili kuhusu hatima ya wanajihadi wawili

Uingereza na Marekani wameanza majadiliano kuhusu hatima ya wanajihadi wawili, raia wa Uingereza, walio na uhusiano na kundi la Islamic State, waliohusika katika mateso na mauaji ya mateka kutoka nchini za Magharibi nchini Syria, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza, Amber Rudd, amesema.

Alexanda Kotey na El Shafee Elsheikh walikamatwa mnamo mwezi Februari na waasi wa Syria wa kundi la SDF.
Alexanda Kotey na El Shafee Elsheikh walikamatwa mnamo mwezi Februari na waasi wa Syria wa kundi la SDF. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Alexanda Kotey na El Shafee Elsheikh walikamatwa mnamo mwezi Februari na waasi wa Syria wa kundi la SDF. Walikuwa miongoni mwa kundi la watu wanne ambao wanaojulikana kama "Beatles".

"Tumeamua kabisa kwamba wanapaswa kuhukumiwa, watu hawa wanapaswa kujibu makosa yao mbele ya mahakama," Amber Rudd ameiambia BBC.

Amber Rudd aliongeza kuwa bado haijajulikana wapi watahukumiwa lakini anashirikiana na Marekani ili kuhakikisha kuwa wanafikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Mawaziri wa ulinzi kutoka nchi kadhaa walioshiriki katika vita dhidi ya kundi la IS walikutana wiki iliyopita mjini Roma bila kufikia makubaliano kuhusu hatima ya wapiganaji wa kigeni wanaozuiliwa Syria.

Katika mkutano huo walijadili kuhusu kurejeshwa nyumbani kwa wapiganaji hao ili waweze kuhukumiwa.

Waziri wa Ulinzi wa Uingereza Gavin Williamson, hata hivyo, amesema hapendelei wanajihadi hao wawili kurudi Uingereza.

Mwanajihadi maarufu zaidi wa "Beatles", Mohammed Emwazi, anayejulikana zaidi kwa jina lake la utani la "Jihadi John", aliuawa mnamo mwezi Novemba 2015 katika mashambulizi ya angani mjini Rakka. Alionekana katika video kadhaa akiwakata vichwa wafungwa, ikiwa ni pamoja na mwaandishi wa habari wa Marekani James Foley.

Mbali na James Foley na mateka wengine kutoka nchi za Magharibi waliuawa, ikiwa ni pamoja na Mmarekani Steven Sotloff. "Beatles" walikuwa waliweza kuwachikilia mateka raia wa Ufaransa Nicolas Hénin, Pierre Torres, Didier Francois na Edouard Elias, ambao waliachiwa huru mnamo mwaka 2014.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.