Pata taarifa kuu
UBELGIJI-UFARANSA-UGAIDI-USALAMA

Kesi ya mtuhumiwa wa mwisho wa mashambulizi ya Paris kusikilizwa Ubelgiji

Maafisa wa Usalama jijini Brussels Ubelgiji wamesema jiji hilo litakuwa katika tahadhari ya hali ya juu hii leo Jumatatu, siku ambayo kesi ya ugaidi inayomkabili mtuhumiwa wa mwisho wa mashambulizi ya Paris mwaka 2015, Salah Abdeslam, itasikilizwa huko Brussels.

Mahakama ya Brussels ambapo kesi ya kwanza ya Salah Abdeslam, mtuhumiwa wa mwisho wa mashambulizi ya Paris itasikilizwa.
Mahakama ya Brussels ambapo kesi ya kwanza ya Salah Abdeslam, mtuhumiwa wa mwisho wa mashambulizi ya Paris itasikilizwa. REUTERS/Francois Lenoir
Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya ulinzi wa taifa vvimetakiwa kuwa makini katika maeneo mbalimbali na mji mkuu wa Ufaransa, wakati mamia ya vikosi vya usalama wa Ubelgiji watalinda jengo la mahakama.

Abdeslam, raia wa Ufaransa mwenye asili ya Morocco anakabiliwa na kosa la kujaribu kuwaua maafisa kadhaa wa Ubelgiji katika mazingira ya kigaidi na kubeba silaha zilizozuiliwa katika mazingira ya kigaidi.

Ubeligiji ilikumbwa na mashambulizi ya kigaidi na kusababisha vifyo vya watu wengi na wengine wengi kujeruhiwa.

Makundi ya kigaidi hasa, kundi la Islamic State kwa miaka kadhaa limetishia kushambulia katika nchi Ulaya na Marekani, hasa nchini zinazojumuika katika muungano wa kimataifa unapambana kivita dhidi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.