Pata taarifa kuu
UHISPANIA-CARLES-SIASA

Mvutano wa kisiasa waendelea Catalonia

Catalonia inaendelea kukabiliwa na mvutano wa kisiasa, wakati ambapo wanaharakati wanaotetea kujitenga kwa eneo hilo wanaendelea na mpango wao wa kumuapisha Carles Puigdemont kama kiongozi wa Catalonia.

Aliyekuwa Kiongozi wa Catalonia Carles Puigdemont.
Aliyekuwa Kiongozi wa Catalonia Carles Puigdemont. Tariq Mikkel Khan/Scanpix Denmark via Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mjadala mkubwa unatarajiwa kuanza leo mchana katika mahakama Catalonia.

Rais aliyetimuliwa kwenye wadhifa wake na serikali kuu ya Madrid ni mgombea pekee katika uongozi wa eneo la Catalonia wenye wakazi milioni 7.5. Bunge la Catalani linatazamia kujadili leo alaasiri kuhusu kuwania kwakekwenye nafasi hiyo.

Wakati huo huo, wafuasi wake wanatarajia kuandamana karibu na jengo la bunge, huku wakitakiwa kuvaa fulana zenye picha ya kiongozi wao.

Haijulikani kama Bw Puigdemont atashiriki maandamano, ao ataonekana hadharani akiwa na wabunge. Kuna hatari ya kukamatwa, baada ya miezi mitatu akiwa uhamishoni nchini Ubelgiji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.