rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Uhispania Mariano Rajoy

Imechapishwa • Imehaririwa

Puigdemont awasili Denmark

media
Rais wa zamani wa Catalonia Carles Puigdemont akiwasili Denmark Jumatatu Januari 22, safari yake ya kwanza nje ya Ubelgiji tangu alipotoroka nchi yake mwezi Oktoba mwaka 2017. REUTERS/Scanpix Denmark/Tariq Mikkel Khan

Mahakama Kuu ya Uhispania imefutilia mbali leo Jumatatu ombi la Mwendesha Mashtaka Mkuu la kurejesha mara moja waranti wa kukamatwa rais wa zamani wa Catalonia Carles Puigdemont, ambaye anafanya ziara yake chini Denmark.


Hii ni ziara yake ya kwanza nje ya Ubelgiji tangu apewe hifadhi katika mji wa Brussels mwishoni mwa mwezi Oktoba.

Hati ya kwanza ya kimataifa ya kukamatwa iliyotolewa dhidi ya Carles Puigdemont kuhusiana na uchunguzi juu ya jaribio la kujitenga kwa eneo la Catalonia ilifutwa mapema mwezi Desemba.

Katika taarifa yake, Mahakama Kuu imesema kuwa uamuzi kuhusu uwezekano wa kurejeshai hati ya kukamatwa kwa kiongozi huyo wa zamani wa Catalonia hautochukuliwa mpaka bunge laCatalonia litakua limeanza shughuli zake za kawaida.

Carles Puigdemont aliwasili uwanja wa ndege wa Kastrup katika mji wa Copenhagen na alionekana akipanda katika ya gari ndogo. Alialikwa kushiriki katika mkutano ulioandaliwa na Idara ya Sayansi ya Siasa ya Chuo Kikuu cha Copenhagen.

Uhispania inamshutumu Carles Puigdemont uasi na uchochezi, baada ya kufanyika kwa kura ya maoni ya Oktoba 1 katika eneo la Catalonia, kura ambayo ilidaiwa na viongozi wa Uhispani kuwa ilikua kinyume cha sheria.

Uteuzi wa mgombea aliyechaguliwa kuongoza serikali ya Catalonia ulifanyika leo Jumatatu. Rais mpya wa Bunge la Catalonia, Roger Torrent aliwasilisha jina la Carles Puigdemont kama mgombea katika uchaguzi huo ambao umepangwa kufanyika Januari 31.

Mjadala bado unaendelea. Wafuasi waCarles Puigdemont wamependekeza kwamba anaweza kuongozi Catalonia akiwa nchini Ubelgiji, hoja ambayo rais wa serikali ya Uhispania Mariano Rajoy amesema haikubaliki.