rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Uhispania

Imechapishwa • Imehaririwa

Carles Puigdemont: Naweza kuongoza Catalonia nikiwa Ubelgiji

media
Carles Puigdemont , kiongozi wa Katalonia aliyetimuliwa mamlakani, akiwa uhamishoni Ubelgiji. REUTERS/Yves Herman

Aliyekuwa wa Catalonia Carles Puigdemont amesema anaweza kuongoza Catalonia akiwa Ubelgiji na hivyo kuepuka kuwekwa jela akitudi nchini Uhispania ambako anafuatliwa na vyombo vya sheria nchini humo.


Hivi karibuni serikali ya Uhispania ilitoa onyo kwa mtu yeyote kuongoza Catalonia akiwa mbali na eneo hilo.

Nikiwa jela, sintoweza kuzungumza na watu, kuandika au kupokea wageni ... Njia pekee ni kuendelea kutekeleza majukumu hayo kwa uhuru na usalama." Siwezi kufanya kuchukua hatua kama rais wa (Catalonia) ikiwa nitakua jela, "Puigdemont amesema katika mahojiano kwenye Radio Catalunya kutoka Ubelgiji, ambako yuko uhamishoni na wasaidizi wake kadhaa wa zamani.

"Ni wazi kuwa si hali ya kawaida ambayo tungependa, lakini kwa bahati mbaya itakuwa vigumu sana kutekeleza majukumu hayo nikiwa nchini Uhispania , ambapo tutawekwa jela ," ameelezea.

"Leo hii, miradi mikuu ya biashara, kitaaluma au utafiti pia inaendeshwa hasa kutumia teknolojia mpya" kutoka mbali, ameongeza.

Kauli yake inakuja wakati ambapo Spika mpya wa bunge la Catalonia, Roger Torrent, anasiliana na vyama mbalimbali kwa kumtafuta mgombea urais wa eneo hilo, baada ya uchaguzi wa Desemba 21 ambapo wanaharakati wanaotaka kujittenga kwa Catalonia walishinda viti vingi.

Carles Puigdemont, ambaye alikimbilia Brussels muda mfupi kabla ya kushtumiwa kuanzisha uasi na uchochezi , anatarajia kuteuliwa akiwa mbali na Catalonia,jambo ambalo vyombo vya sheria vya Catalonia vinaona ni kinyume cha sheria.