rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Ufaransa Uingereza Emmanuel Macron Theresa May

Imechapishwa • Imehaririwa

London na Paris kuimarisha ushirikiano katika masuala ya ulinzi

media
Helikopta ya Uingereza ikiegesha kwenye meli kubwa ya Ufaransa Dixmude wakati wa zoezi la kijeshi, Griffin Strike, kati ya Ufaransa na Uingereza. Olivier Fourt/RFI

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anazuru Uingereza leo Alhamisi kwa mkutano na Waziri Mkuu Theresa May. Katika ziara hiyo rais wa Ufaransa atasaini mkataba mpya juu ya suala la wahamiaji, siku moja baada ya rais Macron kuiomba Uingereza kusaidia kukabiliana na tatizo hilo kwa kuwachukua baadhi ya wakimbizi.


Baada ya chakula cha mchana, wawili hao watazuru Chuo Kikuu cha kijeshi cha Sandhurst, kusini magharibi mwa London. Pia watajadili masuala yanayohusiana na ulinzi, mazingira na elimu, serikali ya Uingereza imetangaza.

Kwa mujibu wa ikulu ya Elysee, viongozi hao wawili watasaini "mkataba mpya ambao utakamilisha mikataba ya Touquet", inayotumika tangu mwaka 2004. Mikataba hii iliweka mpaka wa Uingereza katika eneo la Calais, mji uliokua ukiwapa hifadhi wahamiajii wengi kwa kipindi cha miaka kumi. Wahamiaji ambao wamekua wakijaribu kuingia Uingereza.

Macron ambaye alizuru kambi hiyo Kaskazini mwa Ufaransa, alisema wakimbizi 700 wameondolewa katika eneo hilo na kutaka Uingereza kusaidia kukabiliana na tatizo hilo kwa kuwachukua baadhi ya wakimbizi.

Rais Emmanuel Macron alisema kuwa nchi yake haitaruhusu kwa kambi nyingine ya msituni kuwahifadhi wahamiaji kama ile ya Calais.

Macron alitoa matamshi hayo siku ya Jumanne wakati alitembelea eneo la kaskazini mwa nchi na kaongeza kuwa serikali yake itafanya kila linalowezekana kuzuia ongezeko la wimbi la wahamiaji, Lakini pia kutaka mashirika yanayowasafirisha wahamiaji kuwajibika.

- Kuimarisha ushirikiano wa kijeshi -

Emmanuel MAcron na Theresa Maya wanatarajia pia kujadili masuala ya ulinzi. Siku ya Jumatano serikali ya Uingereza ilitangaza kuwa itatuma helikopta tatu zaRoyal Air Force kusaidia vikosi vya Ufaransa katika eneo la Sahel, pamoja na kuongeza msaada wa kifedha zilizotengwa kwa kukabiliana na ugadi katika eneo hilo.

Wakati huo huo, Ufaransa imekubali kushirikisha askari wake mwaka 2019 katika kikosi cha Jumuiya ya kujihami ya nchi za Magharibi (NATO) nchini Estonia ambacho kinaongozwa na Uingereza.

Theresa May na Emmanuel Macron pia watatangaza miradi ya pamoja kuhusu makombora, ikulu ya Elysee imesema.