rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

EU Uswisi

Imechapishwa • Imehaririwa

EU yapendekeza Uswisi kuwa na mahakama maalum ya usuluhishi

media
CJEU itakua na uwezekano wa kutoa maoni juu ya tafsiri ya sheria za Ulaya zinazoongoza soko moja. REUTERS/Arnd Wiegmann

Umoja wa Ulaya umependekeza kuanzisha mahakama maalum ya usuluhishi ili kukabiliana na mgogoro wake na Uswisi, katika mfumo wa mazungumzo yanayoendelea kuhusu mkataba mpya kati ya Brussels na Bern, vyanzo vinavyojihusisha katika mazungumzo vimebaini.


Wazo ni ni kushughulikia hofu ya Uswisi kuruhusu Mahakama ya Umoja wa Ulaya kuchukua hatua kama muamuzi, hoja iliyofutiliwa mbali na chama cha UDC (Democratic Union of the Center), chama cha kwanza chenye wabunge wengi katika bunge la Uswisi.

Mahakama ya usuluhishi itaundwa na maafisa watatu, mmoja aliyechaguliwa na Umoja wa Ulaya, mwingine na Uswisi na wa tatu kwa ridhaa ya pande zote.

Wataalam hao watatu watakuwa na majukumu ya kutatua migogoro ambayo tume iliyopo inayosimamia uhusiano wa nchi hizi mbili haiwezi kutatua kwa maelewano.

CJEU itakua na uwezekano wa kutoa maoni juu ya tafsiri ya sheria za Ulaya zinazoongoza soko moja.

Uswisi, ambayo si sehemu ya Umoja wa Ulaya, imekuwa ikizungumza kwa miezi kadhaa na Brussels kuhusu makubaliano ya pamoja yanayotakiwa kuleta makubaliano ya kimataifa ya nchi 120 yanayosimamia uahusiano wao.

Rais wa Tume ya Ulaya, Jean-Claude Juncker, alighadhibishwa mwishoni mwa mwaka jana kutokana na kujikokota kwa mazungumxzo hayo, huku akidai kuepo na maendeleo mazuri juu ya mkataba mpya mwaka 2018. Maafisa wa Uswisi, hata hivyo, wanakataa kile wanachochukulia kama tarehe ya mwisho iso rasmi.