Pata taarifa kuu
UHOLANZI-HALI YA HEWA

Dhoruba yapiga Uholanzi, watatu wapoteza maisha

Dhoruba kali ilipiga nchini Uholanzi leo Alhamisi, na kusababisha vifo vya watu watatu, huku safari za ndege zikifutwa. Watu walitakiwa kubaki nyumbani.

Kimbunga cha Kitropiki Hanna kilichopiga kunsini mashariki mwa Florida mnamo Septemba 2, 2008.
Kimbunga cha Kitropiki Hanna kilichopiga kunsini mashariki mwa Florida mnamo Septemba 2, 2008. (Photo : Reuters)
Matangazo ya kibiashara

Upepo mkali unaokwenda kilomita 140 kwa saa uling'oa miti ku na kuharibu magari

Watu watatu waliuawa kwa kuangukiwa na miti vitu vizito, polisi imesema.

Safari za ndege kuwasili au kutoka kwenye uwanja wa ndege wa Amsterdam-Schiphol zimesimamishwa kwa muda mfupi. Ndege zisizopungua 260 zililazimishwa kufuta zafari.

Dhoruba hii pia ilizorotesha usafiri kwa kutumia reli na barabara.

Nchini Ujerumani, shirika la reli la Deutsche Bahn imesimamisha safari zake zote katika eneo la Land Kaskazini mwa Westphalia, eneo lenye watu wengi zaidi nchini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.