rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Ufaransa Emmanuel Macron Wahamiaji

Imechapishwa • Imehaririwa

Macron: Tunaomba Uingereza kuwachukua baadhi ya wakimbizi

media
Rais Macron akutana na wakuu wa mashirika ya kutoa misaada kwa wakimbizi katika eneo la Calais tarehe 16 Januari 2018. Denis Charlet / POOL / AFP

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema hataruhusu tena kuja kwa wakimbizi katika eneo la Calais, ambalo limekuwa likitoa hifadhi kwa mamia ya wakimbizi.


Macron ambaye alizuru kambi hiyo Kaskazini mwa Ufaransa, amesema wakimbizi 700 wameondolewa katika eneo hilo na kutaka Uingereza kusaidia kukabiliana na tatizo hilo kwa kuwachukua baadhi ya wakimbizi.

Rais Emmanuel Macron amesema kuwa nchi yake haitaruhusu kwa kambi nyingine ya msituni kuwahifadhi wahamiaji kama ile ya Calais.

Macron ameyatoa matamshi hayo siku ya Jumanne wakati alitembelea eneo la kaskazini mwa nchi na kaongeza kuwa serikali yake itafanya kila linalowezekana kuzuia ongezeko la wimbi la wahamiaji, Lakini pia kutaka mashirika yanayowasafirisha wahamiaji kuwajibika.

Aidha, amewaonya polisi dhidi ya kutumia nguvu dhidi ya wakimbizi hao.

Rais wa Ufaransa alijaribu kujibu baadhi ya maswali yaliyokua yakitolewa na mashirika yanayosaidiwa wakimbizi katika eneo hilo, mashirika ambayo yamekua yakikosoa hatua za serikali ya Ufaransa dhidi ya wakimbizi hao.

Baadhi ya mashirika ya misaada kwa wahamiaji yalisusia mkutano huo: Utopia 56, Auberge na Medecins du Monde yalitangaza siku moja kabla kwamba hayatatuma mjumbe yeyote kuyawakilisha katika mkutano huo.

Lakini Emmanuel Macron ameelezea masikitiko yake kufuatia lawama hizo: "Watu wanaozungumzia kuhusu kunyanyaswa kwa wakimbizi, watu wanaoongelea vibaya polisi ni waongo na wazushi. "