rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Uhispania

Imechapishwa • Imehaririwa

Uchaguzi Catalonia: Vuguvugu linalotaka kujitenga na Hispania lapata ushindi

media
Des soutiens des s├ęparatistes catalans dans les rues de Barcelone, le 21 d├ęcembre 2017. REUTERS/Albert Gea

Vuguvugu linalotaka kujitenga kwenye jimbo la Catalunia nchini Hispania limepata uwingi wa viti katika uchaguzi uliofanyika hapo jana, hatua inayoleta sintofahamu zaidi ya kisiasa katika historia ya taifa hilo.


Huku idadi ya watu waliojitokeza ikivunja rekodi kwa kufikia asilimia 99.9 ya kura zote zilizohesabiwa, uchaguzi huu umerejesha ushindi wa jumla kwa viongozi wa vuguvugu hilo licha ya kuwa walifanya kampeni wakiwa nje ya nchi.

Hata hivyo vyama vya mrengo wa kati kwenye jimbo hilo vimefanikiwa kupata viti binafsi 37 katika bunge lenye viti 135, jambo ambalo licha ya vuguvugi linalotaka kujitenga kuwa na uwingi wa viti vyama hivi vinaweza kuunda Serikali.

Hata hivyo ikiwa vyama vitatu ambavyo haviungi mkono eneo hilo kujitenga vitashindwa kuunda Serikali ya umoja ni wazi viongozi wa vuguvugu hilo watalazika kuunda Serikali jambo ambalo bila shaka utawala wa Madris hautaki litokee.

Kiongozi aliye uhamishoni Carles Puigdemont amewapongeza wafuasi wake huku akisema matokeo haya ni pigo kwa serikali ya waziri mkuu Mariano Rajoy na washirika wake.