Pata taarifa kuu
AUSTRALIA

Gari lawagonga waenda kwa miguu mjini Melbourne katika tukio lililokusudiwa

Gari limewagonga waenda kwa miguu kwenye mji wa pili kwa ukubwa nchini Australia, Melbourne, katika tukio ambalo polisi wanasema lilikuwa la kukusudiwa ambapo watu zaidi ya 14 wamejeruhiwa kati yao wakiwa na majeraha mabaya.

Polisi wakiwa wamesimama mbele ya gari ambalo lilitumika kuwagonga waenda kwa miguu mjini Melbourne, Australia. 21 Desemba 2017
Polisi wakiwa wamesimama mbele ya gari ambalo lilitumika kuwagonga waenda kwa miguu mjini Melbourne, Australia. 21 Desemba 2017 REUTERS/Luis Ascui
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo wamesema kuwa watu walionekana kurushwa juu wakati gari hilo lilipokuwa likiwagonga waenda kwa miguu na hakukuwa na dalili za dereva kusimama.

Idara ya polisi kwenye kituo cha Victoria wamesema kuwa wanawashikiliwa watu wawili akiwemo dereva wa gari ambaye aliwagonga waenda kwa miguu jirani na kituo cha basi chenye watu wengi mjini Melbourne.

Polisi wanasema kuwa “tunaamini kutokana na kile tulichokiona, kuwa tukio lilifanywa kwa makusudi. Lakini hatujui bado chanzo chake,” alisema kamanda wa kituo cha Victoria Russel Barrett.

Hata Barrett hakuweza kugusia ikiwa tukio hili lina uhusiano wowote na ugaidi ingawa amekiri uchunguzi wa awali umaeanza kufanywa.

Vikosi vya uokoaji vimesema viliwachukua watu kadhaa kuwapeleka Hospitali kati yao wakiwa wamejeruhiwa vibaya.

Polisi wametoa wito kwa raia kuchapisha picha zozote ambazo wanaweza kuwa walirekodi wakati wa tukio.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.