rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Myanmar Aung San Suu Kyi Zeid Ra’ad Al-Hussein UN

Imechapishwa • Imehaririwa

UN: Viongozi wa Myanmar watawajibika kwa makosa ya kivita dhidi ya Warohingya

media
Baadhi ya watoto na wazazi wao jamii wa Rohingya wakiwa nchini Bangladesh REUTERS/Susana Vera

Mkuu wa ya haki za binadamu ya umoja wa Mataifa Zeid Ra'ad Al Hussein amesema kiongozi wa Myanmar Aung San Suu Kyi pamoja na mkuu wa majeshi Jenerali Aung Min Hlaing wanapaswa kushtakiwa kwa mauaji ya kimbari kwa kufumbia macho vitendo vya kikatili vilivyofanywa na majeshi ya nchi yao dhidi ya kabila dogo la waislamu wa Rohingya katika jimbo la Rhakine.


Mapema mwezi huu Zeid aliliambia baraza la haki za binadamu la umoja wa mataifa kuwa vitendo vya kikatili dhidi ya warohingya nchini myanmar vinamaanisha kuwa mauaji ya kimbari hayawezi kuepukika.

Aidha amesema mahakama pekee ndiyo yenya uwezo wa kutihibitisha vitendo vya mauaji ya kimbari vilivyotekelezwa nchini humo huku akitaka kufanyika kwa uchunguzi wa makosa ya jinai kufuatia kile alichokiita kuwa ni mashambulizi ya kikatili dhidi ya kundi hilo dogo la kiislamu ambalo linatoka kaskazini mwa jimbo la Rhakine.

Hata hivyo amesema itakuwa kesi ngumu kuitekeleza kutokana na ukweli kuwa iwapo kuna mpango wa kutekeleza mauaji ya kimbari basi hayawezi kutekelezwa kwa kupitia makaratasi wala kwa kutoa maagizo.

Zeid amesisitiza kuwa alimataka Suu Kyi kuchukua hatua ili kuwalinda warohingya miezi sita kabla ya kulipuka kwa unyanyasaji mnamo mwezi Agosti ambapo zaidi ya watu laki sita walikimbilia Bangladeshi.

Aung San Suu-Kyi mwenyewe amekanusha madai kuwa Serikali yake ilifumbia macho utekelezwa wa vitendo hivyo dhidi ya jamii ya Rohingya, akiukosoa umoja wa Mataifa kwa kuinyooshea kidole nchi yake.

Maelfu ya raia wa Rohingya wamekimbilia kwenye nchi jirani ya Bangladesh kukimbia mashambulizi kwenye jimbo la Rakhine.