rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Ufaransa Ajali

Imechapishwa • Imehaririwa

Watoto 4 wapoteza maisha katika ajali ya basi ya shule Ufaransa

media
Les victimes sont des passagers du bus qui transportait des adolescents âgés de 13 à 17 ans. France Bleu Roussillon/REUTERS

Watoto wanne walipoteza maisha na wengine 17 walijeruhiwa ikiwa ni pamoja na 7 ambao wako katika hali mbaya katika ajali ya basi ya shule iliyogongana na treni kusini magharibi mwa Ufaransa.


Watoto hao walikua katika basi hilo lililokua likibibeba watoto walio na umri kati ya 13 na 17. Ajali hiyo ilitokea siku ya Alhamisi Alaasiri karibu na mji wa Millas, katika mkoa wa Pyrénées-Orientales, karibu na mpaka na Uhispania.

Basi ya shule ilikatika vipande viwili baada ya kugongana na treni. "Utaratibu wa kuwatambua watoto waliopoteza maisha na majeruhi umeanza," alisema Waziri Mkuu Edouard Philippe muda mfupi baada ya kuwasili Millas, mji mdogo wa vijijini wenyeji wakazi 4,000.

Amesema kazi ya kuwatambua majeruhi imekua ngumu.

Wapelelezi nchini Ufaransa wanasubiria kumuhoji mwanamke dereva wa basi hilo

Chanzo kilio karibu na uchunguzi kinabaini kwamba mashahidi tayari wamesikilizwa na wengine wameanza kusikilizwa. Sampuli zitachukuliwa ili kuchunguza kama dereva wa basi na dereva wa treni watakua walitumia pombe wakati wakiendesha vyombo hivyo.