Pata taarifa kuu

Hatma ya Carles Puigdemont na viongozi wengine wa Catalonia kujulikana leo

Aliyekua kiongozi wa Catalonia na wasaidizi wake wanne waliofutwa kazi na Uhispania, wanatarajiwa kusikilizwa leo Jumatatu mjini Brussels na jaji anaehusika na kuchunguza kuhusu waranti zilizotolewa na Madrid, baada ya kutangaza uhuru wa eneo lao mwishoni mwa mwezi Oktoba.

Aliekua kiongozi wa Catalonia Carles Puigdemont wakati wa mahojiano na televisheni ya Ubelgiji, RTBF, Brussels Novemba 3, 2017
Aliekua kiongozi wa Catalonia Carles Puigdemont wakati wa mahojiano na televisheni ya Ubelgiji, RTBF, Brussels Novemba 3, 2017 RTBF Television via Reuters
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja wakati ambapo mahkama ya Uhispania inatarajia kutoa uamuzi wake leo Jumatatu kuhusu kuachiwa chini ya masharti ya kusubiri utaratibu wa mahakama au la viongozi kumi wa Catalonia, baada ya kuzuiliwa kwa tuhuma za kukubali kufanyika kwa kura ya maoni iliyopigwa marufuku na serikali kuu ya Uhispania Oktoba 1.

Uamuzi huo utachunguzwa kwa karibu kwa sababu "ukandamizaji" wa serikali kuu ya Uhispania ambao ndio sababu ya kukandamizwa kwa"wafungwa hao wa kisiasa". Hali hiyo inajiri wakati ambapo kambi inayodai uhuru wa Catalonia inaanza rasmi kampeni yake leo Jumatatu kuhusu uchaguzi muhimu wa eneo hilo uliopangwa kufanyika tarehe 21 Desemba.

Mjini Brussels, viongozi hao watano wa zamani wa Catalonia wanaolengwa na hati ya Ulaya ya kukamatwa (EAW), ambao walikimbilia Ubelgiji Oktoba 30, wanasema, kupitia wanasheria wao wa Ubelgiji, kuwa "kesi hiyo ni ya kisiasa".

Jumatatu, wakati wa mjadala kufungwa imepangwa kutoka 9:00 (0800 GMT), wao kupata wenyewe, kwa ajili ya hatua pleadings, hakimu moja ya chumba baraza la mahakama Uholanzi wa mfano wa kwanza katika Brussels ambayo lazima kupitisha hatima yao.

kusikia kwanza tarehe 17 Novemba alikuwa mdogo kwa kuwasilisha makosa tano kutambuliwa na hakimu Kihispania, ambayo mwendesha mashtaka hakuwa na kujificha Uhifadhi yake kwa kuomba maombi kwa ajili ya utekelezaji "ubaguzi" MFA.

Uhispania inataka viongozi hao wa zamani wa Catalonia wahukumiwe kwa kosa la uasi na uchochezi. Kosa ambalo hukumu yake ni kifungo cha miaka 25.

Lakini sasa uasi na uchochezi ni makosa ambayo hayamo kwenye orodha ya makosa 32 ya jinai yanayotumiwa kwa utekelezwaji wa kukamatwa kwa watuhumiwa katika Umoja wa Ulaya, kulingana na utaratibu ulioanzishwa na Umoja wa Ulaya mwaka 2002, ili kuruhusu kumkabidhi mtuhumiwa kwa nchi mojawapo mwanachama wa Umoja wa Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.