Pata taarifa kuu
EU-UHISPANIA-CATALONIA-USALAMA

EU kutoingilia mzozo wa Uhispania kuhusu uhuru wa Catalonia

Umoja wa Ulaya umesema hauwezi kuingilia mzozo wa kujitenga kwa jimbo la Catalonia nchini Uhispania. Mvutano kati ya Uhispania na viongozi wa Cataloni unaendelea.

Angela Merkel (kushoto), Theresa May (katikati) Na Emmanuel Macron (kulia)  Brussels tarehe 19 Oktoba 2017.
Angela Merkel (kushoto), Theresa May (katikati) Na Emmanuel Macron (kulia) Brussels tarehe 19 Oktoba 2017. REUTERS/Yves Herman
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Baraza la Umoja huo Donald Tusk amesema Umoja huo hauwezi kuingilia mvutano huo au hata kwenda kutoa ushauri.

Tayari uongozi wa Uhispania umesema kuwa unaanza mikakati ya kuwawekea vikwazo viongozi wa Catalonia ambao wamesisitiza kuwa wanataka kujitenga.

Mapema wiki jana serikali kuu ya Uhispania ulitishi kufuta kujitawala kwa jimbo la Cataloni kama kiongozi wa eneo hilo Carles Puigdemont hataweka wazi tangazo lake la uhuru.

Bw Puigdemont alikua alipewa muda hadi Alhamisi awe ameweka wazi au kufuta tangazo lake la uhuru wa jimbo la Catalonia, la sivyo mamlaka ya kujitawala kwa jimbo hilo yatafutwa na kuwekwa chini ya mamlaka ya serikali kuu ya Uhispania.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.