Pata taarifa kuu
AUSTRIA-SIASA

Austria yampata kiongozi mwenye umri mdogo duniani

Mwanasiasa mweye umri wa miaka 31 Sebastian Kurz, kutoka chama cha People's Party, anatarajiwa kuwa kiongozi mpya wa nchi ya Austria.

Sebastian Kurz alishinda uchaguzi wa bunge nchini Austria tarehe 15 Oktoba 2017.
Sebastian Kurz alishinda uchaguzi wa bunge nchini Austria tarehe 15 Oktoba 2017. VLADIMIR SIMICEK / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kurz atakuwa kiongozi mwenye umri mdogo zaidi baada ya chama chake kuonekana kushinda Uchaguzi wa wabunge nchini humo, lakini huenda akaingia kwenye mazungumzo ya kisiasa kuunda serikali ya pamoja.

Akiwahotubia wafuasi wake, Kurz ambaye alikuwa Waziri wa Mambo ya nje akiwa na umri wa miaka 27, amesema atawatumikia raia wa nchi yake kwa nguvu zote.

Haijulikani iwapo atafikiria kuunda serikali ya muungano na chama kinachopinga uhamiaji Freedom Party, kilichoibuka nafasi ya tatu kwa kishindo katika uchaguzi huo.

Bw. Kurz amefananishwa na viongozi vijana wa Ufaransa na Canada, Emmanuel Macron na Justin Trudeau.. Na alipewa jina "Wunderwuzzi" linalomaanisha mtu anayeweza kutembea juu ya maji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.