rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Uhispania Siasa Ulaya

Imechapishwa • Imehaririwa

Waandamanaji nchini Uhispania wapinga uhuru wa Catalonia

media
Waandamanaji jjini Madrid wanaopinga uhuru wa Catalonia Oktoba 8 2017 REUTERS/Juan Medina

Maelfu ya raia wa Uhispania wamekuwa wakiandamana jijini Madrid kushinikiza Umoja wa nchi hiyo, wiki moja baada ya wakazi wa eneo la Catalonia kupiga kura ya maoni ya kutaka kujitawala.


Mbali na jiji Kuu Madrid, maandamano hayo yameshuhudiwa pia mjini Barcelonia katika jimbo la Catalonia ambalo viongozi wake wamesema hivi karibuni watajitangazia uhuru wao.

Wakiwa wamebeba bendera ya Uhispania, waandamanaji hao wamesikika wakiimba na kusema wanataka taifa moja na umoja wa Wahispania.

Pamoja na maandamano hayo, Waziri Mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy amesema Uhuru kura ya maoni ya wakazi wa jimbo la Catalonia kujitenga, haina maana yoyote na haitambuliki.

Rajoy ameliambia gazeti la El Pais kuwa, hatasita kufuta sheria ya eneo la Catalonia kujifanyia maendeleo yake na kuwa na uongozi wa kikanda.

Hata hivyo, uongozi wa Catalonia umesema kuwa wiki ijayo utatangaza uhuru wa eneo lao baada ya wakaazi wa jimbo hilo wiki iliyopita kuamua kuwa wanataka kujitawala wenyewe.